Thomas Rosicky |
Kiungo mchezeshaji
wa Arsenal ambaye alikosekana katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya Euro
2012 ambapo walichapwa na Ureno na kufungwa anafikiria sasa kuachana na soka la
kimataifa.
Katika mchezo
wa robo fainali hakuwepo kutokana na kusumbuliwa na msuli na anaona hakuna haja ya kuendelea kucheza
soka la kimataifa baada ya kucheza kwa takribani miaka 12.
Kikosi cha
kocha Michal Bilek kimeondoshwa katika michuano ya Euro 2012 jana katika mchezo
wa robo fainali kwa kufungwa bao 1-0 na Ureno mjini Warsaw naye akisema hadhani
kama ataendelea na jukumu la kimataifa akilitumikia taifa lake la Jamhuri ya Czeck
maaruku kama “Narodak”.
Amenukuliwa akisema
"najua
mimi si kijana tena nimekuwa na tatizo la afya hivyo niko katika kipindi cha
kufikiria, ningependa kuendelea lakini mimi si pumbavu najua kuwa umri
umekwenda."
Rosicky ambaye
ana umri wa miaka 31 jana alilazimika kukaa katika benchi akishuhudia goli la Cristiano
Ronaldo akifunga goli la kichwa kunako dakika ya 79 ya mchezo huo.
Amenukuliwa akikubali
kuwa Ureno maarufu kama “Seleccao” walikuwa wazuri lakini wanapaswa kujivunia
jihada zao zilizo wafanya kufuzu toka katika kundi lililokuwa na timu ngumu za Russia,
Poland na Greece.
No comments:
Post a Comment