Kiungo mahiri wa klabu ya Yanga Haruna Niyonzima aliyoko nchini Rwanda alikokuwa aanakitumikia kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda katika michezo miwili ya kuwania kufuzu fainali ya kombe la dunia 2014 nchini Brazil na pia fainali za mataifa ya mwaka 2013 nchini Afrika kusini anatarajiwa kurejea nchini ndani ya siku mbili zijazo kujiunga na wachezaji wenzake wa Yanga kwa ajili ya maandalizi ya kombe la Kagame ujao.
Haruna ambaye ni kipenzi cha mashabiki wa klabu ya Yanga amefanya mazungumzo na ROCKERSPORTS na kusema kuwa amemaliza majukumu yake ya kitaifa nchini Rwanda na anajipanga kurejea nchini ndani ya siku mbili zijazo tayari kutoa huduma yake ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake katika makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Niyonzima amesema amefurahishwa na usajili unaoendelea katika klabu yake huku akisema ana imani na wachezaji wapya wanaosajiliwa na klabu kwasasa na kwamba uwezo wa kiungo wa pembeni wa Nizar Khalfani anaufahamu na anadhani Yanga sasa itakuwa na viungo imara watakao unganisha kikosi katika michezo mbalimbali.
hata hivyo amekanusha taarifa za hivi karibuni kuwa alikuwa akifanya kazi ya kuisaidia Yanga kusaka wachezaji toka Rwanda isipokuwa aliwahi kushawishi Yanga kuwasajili baadhi ya wachezaji ambao hata hivyo hakutaka kuwataja majina yao ambapo klabu ilimuahidi kuyashughulikia maoni yake.
No comments:
Post a Comment