Tom
Saintfiet amezaliwa March 29 mwaka 1973 huko Mol nchini Belgium.
Ni meneja wa
chama cha soka nchini Meneja na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Belgium.
alikuwa ni mchezaji wa soka kati ya mwaka 1983 na 1997 kabla ya kuwa meneja
akiwa na umri wa miaka 24 akiwa ni meneja mdogo kuwahi kutokea nchini Belgium.
Saintfiet amefundisha soka katika mataifa mbalimbali
ikiwemo Belgium, Qatar,Ujerumani Germany,visiwa vya Faroe, Finland na uholanzi .
Pia amefanya kazi barani Afrika ambapo amekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa za Namibia na Zimbabwe. kabla ya kuwa kocha mkuu
wa timu ya taifa Namibia, Saintfiet alikuwa meneja wa timu ya ligi kuu ya
nchini Finland ya RoPS Rovaniemi. Mwaka 2002Tom Saintfiet ameifundisha timu moja ya
visiwa vya Faroe ya B71 ambayo ilimaliza ligi katika nafasi ya pili katika ligi
ya nchi hiyo mwaka huo.
baadaye
akaelekea kuifundisha Al-Ittihad Sports Club ya nchini Qatar ambayo sasa inatambulika kama Al-Gharafa
Sports Club. mwaka 2004 alipata nafasi ya kuifundisha timu ya taifa ya vijana(
chini ya miaka 17) ya nchini Qatar ambayo ilifanikiwa kushika nafasi ya tatu
katika vijana barani Asia na kufuzu kucheza fainali za vijana za shirikisho la
soka dunaini FIFA kwa wachezaji wenye umri huo(17 FIFA World Championships).
Kuelekea
katika fainali za kombe la dunia mwaka 2010 (FIFA World Cup 2010) , Saintfiet alikuwa
ni miongozi mwa makocha waliopendekezwa na shirikisho la soka nchini Nigeria
kuifundisha timu ya taifa hilo maarufu Super Eagles fainali ambazo baadaye
zilifanyika nchini Afrika kusini.
Namibia
Saintfiet alianza kuifundisha timu ya taifa ya
Namibia kwa mafanikio akipata ushindi dhidi ya Comoros na timu ya taifa ya Malawi(The
Flames) kisha kupata sare dhidi ya Lesotho katika michuano ya Cosafa maarufu
kama ‘Cosafa Senior Challenge Cup’ nchini Afrika kusini July 2008.
Namibia iliondoshwa
katika robo fainali na waliokuwa wenyeji Afrika kusini(BafanaBafana). Mafanikio
ya Saintfiet ni pamoja na ushindi wa mabao 4-2 mwaka 2010 mchezo wa kuwania
kufuzu kombe la dunia pamoja na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Congo DR mchezo
wa kirafiki.
Siku tatu
baada ya sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Lebanon April 2009, Namibia kwa mara
nyingine tena ilipata sare nyingine ya 0-0 ugenini dhidi ya Angola.
matokeo
mengine ya mafanikio Arguably his most ni kule mjini Durban,pale Namibia ilipokwenda
sare ya bao 1-1 dhidi ya Afrika Kuisni.
Namibia ilikuwa
imeshinda mchezo mmoja tu kabla ya Saintfiet kuwasili nchini humo katika jumla
ya michezo 12 iliyocheza.
Baada ya mafanikio
hayo vyombo vya habari vilianza kumwita kwa jina la utani "The Saint"
na huku gazeti moja likimwita "The Messiah".
Zimbabwe
baada ya kuwepo na taarifa zilizo muhusisha na
kazi nchini Zimbabwe , Sainfiet akafanikiwa miongoni mwa makocha 15 waliomba
kazi nchini humo kupata kazi hiyo na kusaini mkataba wa miaka 4 na shirikisho
la soka la nchi hiyo ZIFA October 2010.
Mwezi November, mamlaka ya uhamiaji nchini Zimbabwean
ilikataa kutoa kibali cha kazi kumruhusu kocha huyo wa Warriors Saintfiet ambaye
baada ya ZIFA ililazimika kusaka kibali cha muda.
October 10 Zimbabwe
ilicheza na Cape Verde mjini Harare mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa
ya Afrika 2012 na kwenda sare ya bao 1-1.
Sainfiet aliendelea kutoa mafunzo kwa timu yake licha ya kuambiwa kuondoka
katika kambi ya timu hiyo kutokana na kukosa kibali cha kufanya kazi nchini
humo.
Akiwa nchini
Namibia alikokuwa akiishi , Saintfiet, alitengeneza mipango yake ya kiufundi
kwa ajili ya timu ya taifa ya Zimbabwe na kutaja kikosi cha timu ya taifa
ambacho kiliichapa Mozambique mabao 3-1 katika mchezo uliofuata.
Baada ya
maombi ya kibali cha kazi kushindikana basi ikalazimika Saintfiet kuachana na
kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya Zimbabwe December 2010.
Shabab Al Ordon
Mwishoni mwa December 2010, Tom alisaini
mkataba wa miezi 4 Month na mabingwa wa mwaka 2007 wa taji la AFC Cup, Shabab
Al Ordon.
Kwa mara
nyingine tena alifanikiwa kusuka eneo la ulinzi la timu hiyo ambayo iliruhusu
bao moja katika jumla ya michezo mitano na Saintfiet akiwa kocha mkuu. Baada ya
michezo sita alipata matokeo ya ushindi katika michezo mitatu na sare tatu.
Kutokana na matatizo ya mahitaji yake kutokutimizwa kama ilivyo tatikana
aliamua kuondoka Shabab Al Ordon baada ya kuifikisha katika nafasi ya pili
katika msimamo wa ligi bila ya kufungwa.
Ethiopia
Baada ya maombi ya timu tatu za taifa ,
Saintfiet alitajwa kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ethiopia May 2011. Mkataba
wa muda mfupi ulikubaliwa na Saintfiet alianza mchezo wake wa kwanza siku kumi
baadaye.
Ethiopia kuelekea
katika mchezo dhidi ya Nigeria kampeni ya kucheza mataifa ya Afrika 2012, ililazimika
kucheza dhidi ya Argentina ambapo ilifungwa mabao 4-1 siku nne kabla ya mchezo
huo na baadaye ikaichapa Ethiopia 4-0 katika mchezo wa kufuzu AFCON nchini
Nigeria mbele ya watazamaji 30,000 ambao walikuwa wakitazama mchezo wa kwanza
wa Saintfiet na kuridhishwa na kiwango cha Ethiopia ambao mpaka mapumziko
walikuwa sare ya bao 1-1.
Baada ya mchezo
kocha wa Nigeria Samson Siasia alikaririwa akisema ameshangazwa hali ya nidhamu
ya mchezo ilionyeshwa na Ethiopia. Pamoja na mafaniko yake yote bado Thom
aliamua mwenyewe kujiuzulu ukocha October 28 2011.
March 28 2012 kocha huyo raia wa Belgium Tom Saintfiet alipewa
mkataba wa miaka minne kama mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la soka la
nchini Nigeria ,hata hivyo mkataba wake ulivunjwa mwezi June.
Sifa Binafsi
Saintfiet ana leseni ya UEFA Pro Licence, ambayo aliipata mwaka 2000.
Kati ya 2006 2007 alikuwa ni mkurugenzi wa
ufundi wa FC Emmen (ligi daraja la
kwanza ya Uholanzi) na pia alifanya kazi kama mshauri wa soka katika shirikisho
la soka la Kazakhstan.
Alifanyakazi pia kama mchambuzi wa mpira wa
miguu katika Television za kuonyesha mpira wa miguu za nchi za Belgium , Afrika
kusini na Namibian pia kama mkalimani wa DFB. amesomea mambo saikolojia katika
michezo na saikolojia ya uchumi.
Saintfiet anazungumza lugha nyingi ikiwemo
kidachi, Kingereza, kifaransa, kijerumani, lugha ya Faroese na ana uwelewa
kiasi katika lugha za kiarabu , kiafrikana na kispanish.
Ni mwandishi mzuri pia wa makala . Katika
fainali ya kombe la dunia za FIFA mwaka 2010, Saintfiet aliandika makala kwa
ajili ya vyombo vya habari vya nchini Belgium (Sport/Voetbal Magazine) na vile
vya nchini Japan.
ni kocha anaefaa yanga iwapo watakuwa na nia ya dhati ya mafanikio.Aachwe atengeneze timu,alipwe maslahi yake kwa wakati,wachezaji walipwe maslahi yao kwa wakati,timu ipate huduma za msingikiutawala na kiufundi kama atakavyohitaji kocha na kwa kuzingatia uwezo wa klabu,apewe muda wa kutosha kutengeneza timu ya ushindi itakayodumu katika kiwango cha juu,na apewe wasaidizi wazuri wasioendekeza majungu,ikibidi kocha wa makipa abadilishwe, arejeshwe Razak Siwa wa kenya
ReplyDelete