Meddie Kagere mshambuliaji mpya Yanga |
Mtihani wa
kwanza wa kocha mpya wa Yanga Thom Saintfiet akiwa kama incharge wa benchi la
ufundi ni hapo kesho atakapo kuwa akiiingoza Yanga kama kocha katika mchezo
dhidi ya JKT Ruvu mchezo wa kirafiki utakao pigwa katika uwanja wa taifa hapa
jijini Dar es Sa laam .
Yanga ambayo
imefanya usajili ambao umewapendeza mashabiki wake itakuwa ikionyesha soka yake
kwa mara ya pili baada ya usajili kuanza lakini mara hii ikiwa chini ya
Mbelgiji Saintfiet kwa mara ya kwanza.
Mbelgiji
huyo ambaye anasafari ya kuifundisha yanga miaka miwili ya mkataba wake amekuwa
akifurahia kikosi chache kilicho sajiliwa na kamati ya Usajili chini ya Salum
Rupia akisaidiana na Seif Ahmed na Abadalah Bin Kleb bila shaka kitaonyesha
kandanda ya matumaini kwa mashabiki wake katika uwanja wa Taifa hiyo .
akizungumzia
mchezo wa kesho afisa habari wa yanga Luis amesema wanatarajia kuonyesha
wachezaji wengine wawili ambao bado kuonekana ambao wameorodheshwa katika
orodha ya wachezaji wapya akiwemo Meddie kagere.
Niyonzima kiungo wa Yanga |
katika
mchezo dhidi ya mabingwa wa soka wa Uganda Express mchezo ambao Yanga ilipata
ushindi wa mabao 2-1 , yanga ilimkosa kiungo wake hodari Haruna Niyonzima hivyo
basi huenda raha ya mchezo wa kesho ikachagizwa na kiungo huyo kwa upande mwingine.
No comments:
Post a Comment