Anton
Ferdinand ameieleza mahakama siku ya Jumatatu kwamba 'ningelikerwa sana' na
matamshi ya ubaguzi wa rangi kama ningelimsikia John Terry akitamka maneno hayo.
John Terry,
mwenye umri wa miaka 31, na ambaye ni mchezaji soka wa Chelsea na vile vile
timu ya taifa ya England, anashtakiwa kwa madai kwamba alimtukana Anton
Ferdinand, kwa kutumia lugha ya ubaguzi wa rangi katika mechi uwanjani, madai
ambayo John Terry ameyakanusha.
Inadaiwa
Terry, nahodha wa timu ya Chelsea, alitamka maneno hayo dhidi ya mlinzi wa QPR,
wakati timu hizo zilipopambana katika uwanja wa QPR wa barabara ya Loftus,
mwezi Oktoba.
Kesi hiyo
inatazamiwa itaendelea kwa siku tano katika mahakama ya Westminster, mjini
London.
Ikiwa Terry
atapatikana na hatia, hukumu kali zaidi itakuwa ni kutozwa faini ya pauni
2,500.
Ferdinand
alisema mahakamani kwamba "wakati mtu anapoleta suala la rangi katika
mchezo, huwa amezidisha matusi na kuyafikisha hatua nyingine".
Inadaiwa
kwamba mlinzi huyo wa Chelsea alimuita mwenzake mweusi, na akitumia maneno pia
yaliyohusishwa na ngono.
Mtaalamu wa
lugha ya kutafsiri yaliyosema kwa kuangalia mdomo, Susan Whitewood,
alithibitisha kwamba matamshi yasiyofaa yalitumiwa na Terry.
Ferdinand
aliielezea mahakama kwamba awali hakudhani lugha ya ubaguzi wa rangi ilitumika.
Lakini baada
ya mechi, rafiki yake wa kike alimchezea video iliyokuwa katika tovuti ya YouTube,
na baada ya hapo, alibadilisha nia na kuamua kuchukua hatua za kisheria.
Ferdinand
alisema kwamba kama moja kwa moja angelitambua Terry alimtukana uwanjani kwa
kutumia matamshi hayo, basi papo hapo angeliwaarifu maafisa waliyosimamia mechi
hiyo.
No comments:
Post a Comment