KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, September 13, 2012

KIMATAIFA:RONALDO KUSEM A NA RAIS PEREZ NA WAKUU WA FA WAOMBA RADHI JANGA LA Hillsborough 1989..


Cristiano Ronaldo kukutana na Rais wa Real Madrid Florentino hii leo

Cristiano Ronaldo anatarajiwa kukutana na Rais wa Real Madrid Florentino Perez hii leo kujaribu kuzungumzia juu ya hali ya mambo ndani ya mabingwa hao wa Liga.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno aliweka wazi wakati wa kipindi kif kuwa hana raha na masha yake ndani na Santiago Bernabeu kutokana na sababu alizo ziita sababu za kukosekana kiutaaalam kiasi kusemwa mengi juu ya hali yake hiyo ya kutokakuwa na furaha.

Ronaldo alirejea Madrid hapo jana baada ya kumaliza majukumu ya kitaifa akiwa na timu yake ya taifa ya Ureno ambapo mara baada ya kurejea alikutana ana kwa ana na kocha Jose Mourinho wakiwa katika mazungumzo kabla ya kuelekea kwenye uwanja wa mazoezi.
Sasa anatarajiwa kukutana na Perez , ili kuweka wazi yanayo msibu wakati Madrid ikisaka suluhisho la tatizo la mshambulizi huyo.

FA yaomba radhi juu ya janga la Hillsborough
 
  Mwenyekiti wa chama cha soka nchini Engalnd David Bernstein ameomba radhi kufuatia maafa yaliyotokea Hillsborough.
Mashabiki wa Liverpool wamekuwa wakitoa heshima zao na kutoa maua ambayo yamekuwa yakipelekwa katika uwanja wa klabu hiyo Anfield.

Maneno ya kuomba radhi yamekuja kufuatia kundi la  mashabiki wa klabu hiyo linalo tambulika kama ‘Hillsborough Family Support Group’ kutaka bodi ya utawala ya chama cha soka cha England kuomba radhi.
FA iliruhusu mchezo wa nusu fainali wa kombe la FA mwaka 1989 ufanyike ambapo jumla ya watu 96 walipoteza maisha katika uwanja wa Sheffield licha ya kuwa kulikuwa hakuna kibali cha kuruhusu mchezo huo kufanyika katika uwanja huo ambao ujaa maelfu ya watazamaji kiasi kuleta madhara makubwa.

"Tunaomba radhi kwa janga hili kutokea katika uwanja ambao FA iliuteua. Mchezo huu ulichezwa katika michuano ambayo inaandaliwa na FA yenyewe, kwa niaba ya FA , ninaomba radhi na tungependa kutoa rambirambi kwa familia zote ambazo zimepoteza wapendwa wao na kila mtu anae ungana na mji wa Liverpool na klabu ya Liverpool yenyewe ".
"Hili halita tokea tena. Hakuna mtu atakae poteza maisha atakapo kuwa amekaa akiangalia mpira , na ni suala la kujutia na huzuni kubwa imetokea siku nyingi zilizopita na waliopoteza maisha kutambulika na ukweli kuzungumzwa."

Mapema hii leo, FA ilitoa taarifa ambayo ilihusu machapisho ya ripoti ya uchunguzi ya janga hilo iliyo tambulika kama ‘Hillsborough Independent Panel's report’ ambayo ilisema kuwa janga la janga kubwa ambalo halitasahaulika ambalo lilitokea April 15, 1989.

No comments:

Post a Comment