KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, September 13, 2012

TISHIO LA NYAU SIMBA LAYEYUKA, DOLE GUMBA LA YONDANI LAPELEKWA POLISI.

 
 
Kamati ya utendaji ya mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara klabu ya Simba imekubali kuirejesha katika ligi kuu ya Tanzania Bara timu yao baada ya kikao cha kamati hiyo kukutana na kujadili taarifa ya kamati ya maadili nidhamu na hadhi ya wachezaji ya Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF chini ya mwenyekiti wake Alex Mgongolwa.
Kamati ya Mgongolwa mapema wiki hii ilitoa taarifa ya maamuzi ya kamati hiyo juu ya masuala ya usajili wenye utata ambapo suala lilivuta hisia za mashabiki wengi nchini kuhusu usajili wa wachezaji kiungo Ramadhani Chombo Ridondo , mlinzi wa kati king'ang'anizi Kelvin Yondani  na mlinzi wa kati raia wa Congo Mbuyu Twite.

Kamati hiyo iliwahalalisha wachezaji Yondani na Twite kuchezea Yanga ambao ni mabingwa wa kombe la Kagame kwa mujibu wa kanuni za TFF na  FIFA jambo ambalo lilipelekea klabu ya Simba kutishia kujitoa katika ligi kuu na michuano yote inayoandaliwa na TFF.
Akiongea na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya klabu ya Simba , Afisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kamati ya utendaji ya Simba imeamua kurudi katika ligi baada ya kubaini kuwa kujitoa kwao ingetafsiriwa kama klabu hiyo imesusa.

Pia kamati hiyo ya Utendaji imewataka wanachama wa klabu hiyo waliokuwa wamejipanga kwenda mahakamani kuishitaki TFF kuacha kufanya hivyo kwani klabu hiyo imeamua kusonga mbele zaidi kwa kuupeleka mkataba wa Yondani Polisi kupata ukweli kuhusu saini ya kidole gumba cha mchezaji huyo na kutoa majibu ya kama alisaini Simba ama lah.

No comments:

Post a Comment