Mwenyekiti
wa chama cha soka nchini England David Bernstein anatarajia kuzindua sheria
mpya ya kimaadili kwa ajili ya wachezaji wa timu ya taifa ya England.
Hatua hiyo
inafuatia kujitokeza kwa vitendo vya uvunjifu wa nidhamu kutoka kwa wachezaji
wa kimataifa na zaidi akinyooshewa kidole mlinzi Ashley Cole.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na FA ni kwamba kwa mchezaji yoyote atakaye vunja sheria
hiyo basi atasimamishwa kuitumikia timu ya taifa.
Amenukuliwa
Bernstein akisema
"kuna
wachezaji ambao wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa na wanasifa nzuri iliyotukuka na
pia wanatakiwa kuonyesha tabia nzuri ni muhimu "
"na
sheria hii ilipaswa kuletwa miaka mingi nyuma."
“kama kuna mtu atafanya ndivyo sivyo tutakuwa
na uwezo
wa kumuonya au kumsimamisha kucheza soka England”
Cole aliingia
matatizoni baada ya kutuma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa
twitter akikitukana chama cha soka nchini England FA kuelekea kusikilizwa kwa
shauri la mchezaji mwenzake mlinzi John Terry.
("Hahahahaa,
well done #fa I lied did I, #BUNCHOFT***S".)
Lakini hata
hivyo mlinzi huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 31 baadaye aliufuta ujumbe
huo na kumuomba radhi Bernstein kabla ya kukutana jumanne na Prince William wakati
wa hafla ya ufunguzi rasmi wa kituo kipya cha FA kilichopo St George's Park on Tuesday.
Kwasasa bado
mlinzi huyo wa Chelsea ambaye ameitumikia England michezo 98 anakabiliwa na
tuhuma hizo ambapo anatakiwa kujibu tuhuma zake hizo kabla ya saa moja usiku wa
kesho October 11.
MAKAMU WA RAIS FIFA JIM BOYCE ANASEMA KUJIRUSHA KWA WACHEZAJI ENEO LA HATARI KAMA KANSA MCHEZONI
Makama wa
Rais wa shirikisho la soka duniani Fifa Jim Boyce amesema anaamini kitendo cha
kujirusha ndani ya eneo la hatari sasa kimekuwa kama ugonjwa wa kansa.
Boyce
ametoa kauli hiyo baada ya kuangalia mchezo baina ya Liverpool dhidi ya Stoke
mchezo uliochezwa katika dimba la Anfield ambapo alimshuhudia Luis Suarez akijiangusha
ndani ya eneo hilo katika mchezo uliomalizika kwa matokeo ya bila kufungana.
Amenukuliwa
akisema,
"Nimeona
matukio mengi ikiwa ni pamoja na hili la Suarez na kwangu mimi hakuna kitu
isipokuwa ni udanganyifu"
Akaenda mbali kwa kusema,
“hili
linaweza kushughulikiwa na kamati za nidhamu kama inavyofanyika katika vyama vingine na kwamba hiyo ndiyo njia
sahihi ya kufanya”
"Sasa
linakuwa kama ugonjwa wa kansa ndani ya mchezo . Endapo itathibitika kuwa ni
kweli mchezaji kafanya hivyo wanapaswa kuadhibiwa."
Mwezi September,
bosi wa Stoke Tony Pulis alitaka FA kuwaadhibu wale watakao bainika kufanya
vitendo vya kujirusha kwa kusimamishwa michezo mitatu.
Na jumapili
iliyopita akarejea kwa kusema mshambuliaji Suarez alistahili kusimamishwa
michezo hiyo baada ya kujirusha katika mchezo uliochezwa Anfield na kutoa matokeo ya kutokufungana.
Busquets asimamishwa michezo miwili
ya vilabu bingwa ulaya.
Kocha wa Barcelona
Tito Vilanova ataikosa huduma ya Sergio Busquets katika michezo miwili ijayo ya
vilabu bingwa ulaya dhidi ya Celtic kufuatia shirikisho la soka barani ulaya UEFA
kuamua kumsimamisha kiungo huyo kwa michezo miwili kutokana na kufanya ndivyo
sivyo katika mchezo dhidi ya Benfica wiki iliyopita.
Kiungo huyo
wa kimataifa wa Hispania alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi
wa kituruki Cuneyt Cakir baada ya kumchezea rafu mbaya Aguias wa Benfica, katika mchezo ambao Catalans
walishinda kwa mabao 2-0.
Bodi ya
udhibiti na nidhamu ya UEFA imelitazama suala hilo na kulitolea maamuzi ya kwamba Busquets asimame michezo miwili.
Kiungo huyo
mwenye umri wa miaka 24 atakosekana katika mchezo wa kwanza katika uwanja wa nyumbani dhidi
ya Celtic Oct 23 lakini pia atakosekana
katika mchezo wa marudiano wiki mbili baadaye.
Barcelona kwasasa
wako katika kilele cha kundi G wakiwa na alama sita baada ya kushuka dimbani
michezo miwili, ilhali Celtic wako katika nafasi ya pili baada ya kukusanya
alama nne.
No comments:
Post a Comment