Nahodha wa Manchester
United Nemanja Vidic anaamini kuwa iko siku mshambuliaji wa zamani wa United Cristiano
Ronaldo atarejea Old Trafford.
Ronaldo usiku
huu atakuwa akirejea kwa mara ya kwanza Old Trafford akiwa na kikosi cha Real Madrid ambacho
kitakuwa kikikabiliana na kikosi chake cha zamani United katika mchezo wa ligi
ya mabingwa barani Ulaya hatua ya 16 bora.
Vidic, ambaye
amecheza na mreno Ronaldo kabla ya kuihama kwa uhamisho wenye thamani ya rekodi
ya dunia wa pauni milioni £80 na kujiunga katika viunga vya Bernabeu mwaka 2009,
ana matumaini kuwa yeye na mshambuliaji huyo iko siku wataungana tena na
kucheza pamoja chini ya meneja babu Sir Alex Ferguson.
No comments:
Post a Comment