Wladimir
Klitschko atatetea mataji yake ya uzito wa juu ya WBA, IBF na WBO dhidi ya
swahiba wake wa zamani wa mazoezi Francesco Pianeta pambano ambalo litachezwa huko
Mannheim May 4.
Klitschko, raia
wa Ukraine mwenye umri wa miaka 36 atakuwa anatetea kwa mara ya 14 akiwa ubingwa
wa dunia wa uzito wa juu.
Pianeta, ambaye
ni raia wa Italia lakini maskani yake yakiwa nchini Ujerumani hajapoteza hata
pambano moja katika mapambano yake 29 aliyocheza mbali ya kwenda sare pambano
moja.
Amenukuliwa Pianeta
akisema
"Wengi
wanadhamni mimi nitapigwa, lakini ukweli ni kwamba nitamgonga
Klitschko na kuugeuza ulimwengu wa masumbwi."
No comments:
Post a Comment