Real Madrid italazimika kushuka dimbani Old
Trafford ikiwa ndani ya jezi za rangi ya kijani na michirizi miepe kwa lengo kuepuka kufanana rangi na wenyeji wa mchezo huo Manchester United huku wachezaji wakionekana wazi wazi kuwa na wasiwasi na rangi ya jezi hiyo.
Jezi zilizo zoeleka za rangi nyeupe hazita tumiwa na timu hiyo hii leo kutokana na kuepuka kufanana na jezi chaguo la kwanza za United na wakionekana kutokuwa tayari kuvaa jezi nyeusi.
Jezi za rangi ya kijani ambazo zimekuwa zikitumika wakati fulani kwa michezo ya nyumbani hazijashinda hata mchezo mmoja ya ligi isipokuwa michezo ya ligi ya mabingwa Ulaya hatua ya makundi dhidi ya Ajax na Manchester City kabla ya kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Sevilla, mchezo ambao ulianza kumuweka kitimoto Jose Mourinho.
Kufuatia matokeo hayo wachezaji wa timu hiyo wamekuwa wakiamini kuwa kuvaa jezi zenye rangi hiyo ni sawa na kujitia nuksi.
No comments:
Post a Comment