Temeke
imekuwa timu ya kwanza kupata tiketi ya kucheza nusu fainali kwenye michuano ya
mwaka huu ya Copa Coca-Cola baada ya kuing’oa Mjini Magharibi kwa mikwaju ya
penalti.
Mechi hiyo
ya kwanza ya robo fainali imechezwa leo asubuhi (Julai 10 mwaka huu) Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam ambapo hadi dakika 90 za kawaida
zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1.
Mjini
Magharibi ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 79 lililofungwa na Salum Maulid
wakati Abdul Hassan aliisawazishia Temeke dakika ya 90.
Waliofunga
penalti kwa upande wa Temeke ni Baraka Ntalukundo, Khalid Mwendakamo, Mohamed
Dikougwa na Abdul Hassan wakati aliyekosa ni Anwar Kilemile. Waliokosa kwa
Mjini Magharibi ni Abdulrahman Mohamed na Salum Maulid wakati waliofunga ni
Alawi Kombo na Salum Shukuru.
Katika nusu
fainali, Temeke itacheza na mshindi wa mechi ya robo fainali kati ya Kinondoni
na Mwanza itakayochezwa kesho asubuhi (Julai 11 mwaka huu) Uwanja wa Karume,
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment