El Salam Wau ya Sudan Kusini |
El Salam Wau
ya Sudan Kusini na Atletico ya Burundi zinatarajiwa kuwa timu za kwanza
kuwasili nchini kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati
(Kombe la Kagame).
Michuano hiyo
inaanza kutimua vumbi Jumamosi (Julai 14 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam ikishirikisha timu kumi na moja akiwemo bingwa mtetezi Yanga na
makamu bingwa Simba.
Kikosi cha
El Salam Wau ambacho kitawasili kesho alfajiri (Julai 11 mwaka huu) kwa ndege
ya Ethiopia Airlines kikitokea Juba kupitia Addis Ababa, Ethiopia kikiwa na
wachezaji 18 na viongozi saba.
Wachezaji
wanaounda kikosi hicho ni Khamis Leone Uso Wani (nahodha), Adheil Bugwic
Jongkor Bugwic, Edward Joram Simon Julio, Fidel Andrea Fides Fas, Ismael Musa
Juma Ismael, James Anei Matheli Anei, Jervas Ayo Abdalla Ayak, Khamis Doshama
Ulama Andel na Meki Sultan Berema Kuku.
Wengine ni
Moga Emmanuel Androga, Mubarak Mohammed Saleh Omer, Ndili Rabeh Nasir Hozi,
Nizir Rihan Taban Talib, Oliver Paul Kangi Akok, Rabie Mohammed Abubakar
Hassan, Rufino Joseph Uras Ambros, Santino Makuei Uyu Upio, Thomas Rufino
Thomas Diakon.
Nayo
Atletico inatarajiwa kuwasili kesho (Julai 11 mwaka huu) kwa usafiri wa
barabara. Timu hiyo inakuja kwa usafiri wa basi lake ambalo pia italitumia kwa
muda wote itakapokuwa kwenye mashindano.
Wakati El
Salam Wau itafikia kwenye hoteli ya Rungwe iliyoko maeneo ya Kariakoo, Atletico
itakuwa Lunch Time Hotel iliyoko Mabibo.
Timu
zinazotarajiwa kuwasili keshokutwa (Julai 12 mwaka huu) ni Mafunzo ya Zanzibar
kwa boti saa 9 alasiri, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (RDC)
itatua saa 1.20 usiku kwa Kenya Airways. Timu nyingine itakayowasili siku hiyo
jioni ni URA ya Uganda.
No comments:
Post a Comment