WATANGAZAJI KWA ‘SCREEN’ KUBWA KOMBE
LA KAGAME
Wakati wa
michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kuanzia Julai 14-28 mwaka huu, screen kubwa iliyoko uwanjani itatumika kwa
matangazo ya biashara na ujumbe mbalimbali kwa washabiki watakaoshuhudia mechi
hizo.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linakaribisha kampuni na wadau mbalimbali
wanaotaka kuweka matangazo yao wakati wa michuano hiyo itakayoshirikisha klabu
kumi na moja kutoka ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.
Muda wa
kurushwa matangazo hayo yanayotakiwa kuwa kwenye mfumo wa DVD ni kabla ya mechi
kuanza, wakati wa mapumziko na baada ya mechi. Matangazo hayo yanatakiwa kuwa
ya sekunde 60 (dakika moja) au sekunde 30 (nusu dakika).
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM), Fabian Samo
kilichotokea leo asubuhi (Julai 10 mwaka huu).
Samo ambaye
Novemba 13 mwaka jana alichaguliwa kwa kipindi cha pili mfululizo kuwa
Mwenyekiti wa FAM katika uchaguzi uliofanyika wilayani Rorya alikuwa amelazwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam akisumbuliwa na maradhi ya
figo.
Taratibu za
mazishi ya Samo ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu (Internal
Audit Committee) ya TFF ikiwemo siku atakayozikwa bado zinafanywa na familia
yake.
Samo alitoa
mchango mkubwa katika maendeleo ya mpira wa miguu mkoani Mara na Tanzania kwa
ujumla, vitu ambavyo vilichangia kuchaguliwa kwake tena kuiongoza FAM.
Msiba huo ni
pigo kwa familia ya Samo, FAM, TFF na mchezo wa mpira wa miguu kwa ujumla
nchini kutokana na mchango na mawazo aliyotoa kwa kipindi chote alichokuwa kiongozi.
TFF inatoa
pole kwa familia ya marehemu Samo, FAM, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na
uvumilivu katika kipindi hiki cha msiba huo mzito. Pia TFF itatoa ubani wa sh.
200,000 kwa familia ya marehemu kama rambirambi zake.
Mungu aiweke
roho ya marehemu Samo mahali pema peponi. Amina
KOZI YA MAKOCHA WA GRASSROOTS
Kozi ya
makocha wa mpango wa grassroots unaolenga wachezaji mpira wa miguu (wasichana
na wavulana) wenye umri kuanzia miaka 6-12 imeanza leo (Julai 10 mwaka huu)
kwenye ukumbi wa Msimbazi Center, Dar es Salaam.
Wakufunzi
kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ndiyo wanaoendesha kozi
hiyo iliyofunguliwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Angetile Osiah.
Kozi hiyo
itakayomalizika Julai 15 mwaka huu inashirikisha washiriki 35, na mwendelezo wa
ile ya awali iliyofanyika Desemba 14-17 mwaka jana jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment