KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, July 21, 2012

Manchester United iko tayari kumnunua Lucas Moura

Lucas Moura
Manchester United inajipanga kumnunua Lucas Moura kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £32 baada ya klabu yake ya Sao Paulo kugomea ada ya pauni milioni  £27.2m za awali.
Klabu hiyo ya nchini Brazil imedai kuwa United imeonyesha nia ya kuweka kile ambacho klabu hiyo ilichokiita offer muhimu ya euro milioni €35 ambayo ni sawa na pauni milioni £27.2 kwa ajili ya kiungo mshambuliaji huyo kijana kabisa mwenye umri wa miaka 19.
Vyanzo vya habari vimeeonyesha kuwa mashetani wekundu wameweka offer hiyo juzi na kwamba Sao Paulo imesema kiwango hicho kinatosha kukamilisha mipango ya kumuuza mchezaji huyo.
Lucas, ambaye alikuwa ni sehemu ya wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil ambayo iliichapa Great Britain katika mchezo wa kujipima nguvu wa maandalizi ya michezo ya Olympics ijumaa usiku.
Bosi wa United Sir Alex Ferguson alipata nafasi ya kumuona Moura kupitia mchezo huo na kuona kuwa anaweza kuziba nafasi ya Eden Hazard ambaye walikuwa wakimtaka huko nyuma kabla ya kushindwa kunasa saini ambapo Chelsea walifanikisha wakati wa ufunguzi dirisha la usajili.
Imefahamika kuwa kiasi hicho cha pesa kipo kwa ajili kumsaini Lucas lakini pia Uinted haiku tayari kwenda nje ya kiwango hicho kwa maana ya zaidi ya hapo.
United ina imani mchezaji huyo anayezungumza lugha ya kireno atakapo kuwa na wenzake wanaozungumza lugha hiyo kama vile Nani, Anderson na Rafael Da Silva atakuwa na kazi rahisi ya kuelewana na wenzake.

No comments:

Post a Comment