Angelo Henriquez |
Universidad
de Chile confirm Manchester United move for Angelo Henriquez
Mshambuliaji
wa Universidad de Chile Angelo Henriquez anajipanga kuelekea Manchester United
hizi zikiwa ni taarifa toka ndani ya klabu yake.
Kinda huyo
mwenye umri wa miaka 18 anatarajiwa kukamilisha mipango hiyo kabla ya
kumalizika kwa mwezi huu wa August, baada ya kukamilisha vipimo ya afya yake
wiki hii na kuwa mchezaji wa kwanza raia wa Chile kuichezea klabu hiyo.
Henriquez amefunga
jumla ya mabao 10 baada ya kucheza michezo 15 ya ligi ya Chile lakini pia anaichezea
timu ya vijana ya Chile ya Under-20.
Henriquez amekuwa
akionekana kupata ukomavu vizuri katika soka jambo ambalo limemfanya mzee Alex Furguson
kuvutiwa na soka yake.
Taarifa ya
klabu yake imesomeka
"Angelo
Henriquez atajiunga na Manchester United mwezi huu ,"
"mchezaji
yuko safi ‘physically and mentally’ katika kuendeleza soka yake."
Rais wa
klabu yake Jose Yuraszcek amesema "mwakilishi wa Manchester United's
representatives ametuambia ni muhimu kwao kumchukua kijana huyo sasa"
Henriquez,ambaye
ameanza kuitumikia klabu yake mapema mwaka huu amethibtisha juu ya hili na
akisema kwake ni kama ndoto inakuwa kweli.
Imeelezwa
kuwa kijana huyo alikataa mpango wa kuelekea Manchester City kwa ajili ya
kusaini kwa mashetani wekundu.
No comments:
Post a Comment