Benzema:kilichokuwa muhimu hatuja
poteza kwa uruguay.
Karim Benzema |
Karim
Benzema nyota wa Real Madrid amesema sare ya bila mabao dhidi ya mabingwa wa
taji la Copa America si mbaya
Ufaransa haikufanikiwa
kupata bao katika mchezo wao wa kwanza chini ya kocha mpya Didier Deschamps
licha ya kuwa katika ubora lakini mshambuliaji huyo wa Real Madrid anasema
ameridhishwa matokeo ya mchezo huo.
"tulipoteza
nafasi nafasi za wazi lakini si mbaya kwa kuwa hatujafungwa yote kwa yote
ulikuwa ni mchezo wa kiwango cha juu kwetu"
Benzema alikuwa
akiongea na L'Equipe.
Wakati huo
huo kiungo wa Toulouse Etienne Capoue alifurahishwa na kuwa katika kikosi hicho
kwa mara ya kwanza akiitumikia timu ya Taifa ya Uafaransa.
amesema
"pamoja
na kwamba hatukufunga lakini tulicheza vizuri,".
"nikiwa
dimbani kwa mara ya kwanza katika timu ya taifa nimejikia faraja. Didier
Deschamps aliniambia niwe mimi uwanjani nitafurahia mchezo ndivyo ilivyokuwa. imekuwa
poa mimi kuwepo hapa."
Ufaransa
itapambana na Finland katika mchezo mwengine utakachezwa September 6.
Robie Van Persie |
Mshambuliaji
wa Asernal Robie Van Persie anaelekea kukamilisha uhamisho wake wa ada ya pauni
milioni £24 kuelekea Old Trafford usajili ambao unatarajiwa kukamilishwa hii
endapo atakuwa amefuzu vipimo vya afya na makubaliano ya maslahi binafsi.
Endapo
mshambuliaji huyo atakamilisha hilo atakuwa ni mchezaji mwenye gharama kubwa
kuhamia Old Trafford tangu kufanya hivyo mara ya mwisho Dimitar Berbatov mwaka 2008 ambaye ameweka
rikodi katika usajili wa ‘Premier League’.
Van Persie sasa
anakwenda kuungana na Wayne Rooney kujenga safu kali ya ushambuliaji ya United.
Mike Carrick
amepokea kwa mikono miwili juu ya taarifa hizo za ujio wa Persie akisema
"kuna
mtu alidokeza katika chumba cha kubadilishia nguo hukusu Van Persie na kama
itakwenda vizuri itakuwa safi sana," kauli hiyo ya Carrick imekuja baada ya mchezo
wa ushindi kwa England wa mabao 2-1 dhidi ya Italy usiku wa jana "
Ameendelea
kwa kusema alikuwa katika msumu mzuri msimu uliopita na ataboresha kikosi.
Kiungo Tom
Cleverley ameongeza
"ni wazi mchezaji mkubwa atatufanya kuwa
wazuri."
Katika hatua
nyingine meneja wa Manchester United Sir
Alex Ferguson anaamini usajili wa Robin van Persie utampa safu ya ushambuliaji
kali kama ilivyokuwa katika kikosi cha mwaka 1999 ambacho kiliisaidia United
kushinda taji la vilabu bingwa.
Ferguson anamtarajia
mduchi huyo jumatatu katika mchezo dhidi
ya Everton ambapo atajiunga na Wayne Rooney kujenga ‘partnership’ ya wawili
kushambulia nyavu.
Lewandowski: Nasalia Dortmund.
Robert Lewandowski |
Mshambuliaji
wa Borussia Dortmund Robert Lewandowski amekanusha
taarifa za kuondoka katika timu yake hiyo msimu huu .
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Poland ambaye alifunga mabao matatu ‘hat trick’ dhidi ya Bayern
Munich katika mchezo wa fainali wa DFB Pokal mwezi May alikuwa na mchqango mkubwa
kwa Dortmund akifunga jumla ya mabao 22 na kutoa pasi za mwisho za mabao kumi
aliamsha tetesi za kuondoka katika klabu yake na kuelekea kwa Bayern,
Manchester United, Chelsea na Juventus.
Licha ya kiu
yake ya kutaka kuchezea ligi kuu ya Uingereza ‘Premier League’, Lewandowski sasa
ametangaza kuwa atasalia katika ligi ya Ujerumani Bundesliga akiwa na Dortmund.
Dortmund tayari
imetoa taarifa kwa vilabu vinavyo mtaka Lewandowski kuwa hataondoka tena na
atasalia Westfalenstadion mpaka atakapo maliza msimu na mazungumzo na wakala
wake Cezary Kucharski yanatarakiwa kufanyika japokuwa Bayern iko tayari kutoa
offer ya ongezeko la mshahara mnono wa euro €144,000 kwa wiki ili kumpeleka Allianz
Arena.
No comments:
Post a Comment