Victor Ochieng, ambaye ni majeruhi ameachwa katika kikosi cha AFC Leopards ambacho kinakuja nchini kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara ‘Vodacom Tanzanian Premier League’ Simba SC na mchezo mwingine dhidi ya mabingwa wa kombe la Kagame Yanga FC.
Walinda
mlango Patrick Matasi na Barnabas Tiema ni miongoni mwa wachezaji walioko
katika ziara hiyo na watakuwa wakiambatana na walinzi Martin Imbalambala, Eric
Masika, Idrissa Rajab, Jonas Nahimana, Abbass Kiwalabye na Amon Muchiri.
Viungo ni Bernard
Mangoli, Laurent Tumba, Edwin Wafula, Paul Were, Charles Okwemba na Floribert
Tambwe.
washambiliaji
katika kikosi cha kocha Jan Koops ni Jimmy Bageya, Allan Wanga, Oscar Kadenge na
Mike Barasa.
Kikosi hicho
kitakuwa safarini hapo kesho kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza utakaopigwa
jumapili dhidi ya Simba katika uwanja wa Sheikh Amri Abed Kaluta .
Baada ya
mchezo huo Leopards wataelekea Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa pili
dhidi ya Yanga uliopangwa kuchezwa August 22.
Kikosi kamili
Goalkeepers: Patrick Matasi, Barnabas Tiema.
Defenders: Martin Imbalambala, Eric Masika,
Idrissa Rajab, Jonas Nahimana, Abbassi Kiwaalabye and Amon Muchiri.
Midfielders: Bernard Mangoli, Laurent
Tumba,Edwin Wafula, Paul Were, Charles Okwemba and Floribert Tambwe.
Strikers: Jimmy Bageya, Allan Wanga, Oscar Kadenge
and Mike Barasa.
No comments:
Post a Comment