![]() |
Mwenyekiti wa kamati ya katiba ,sheria na hadhi ya wachezaji tff. |
Kuelekea
kuanza kwa msimu mpya ligi kuu ya soka Tanzania 2012/2013, vilabu vyote shiriki
vimewasilisha majina ya wachezaji wao ambapo tarehe ya mwisho ya kuwasilisha
majina hayo ilikuwa ni saa 11 jioni ya jana huo ukiwa ni baada ya kuongezwa
siku tano mbele.
Katika
kuwasilisha majina hayo klabu ya mwisho ilikuwa ni wana Kishamapanda Toto
Afrika ya Mwanza ambao walikamisha idadi kamili ya vilabu vyote kumi na nne.
Akiongea na
waandishi wa habari katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini Angetile Oseah
amesema pamoja na zoezi hilo kukamilika kwa wakati kama ilivyo tangazwa lakini
bado kuna matatizo kadhaa ambayo ofisi yake imeyaona ambayo kimsingi
yatapelekwa katika kamati katiba sheria na hadhi za wachezaji ili kupatiwa
ufumbuzi.
Miongoni mwa
mambo ambayo yameonekana kama ni mkanganyiko ni kujitokeza kwa majina ya baadhi
ya wachezaji katika orodha ya wachezaji wa klabu mbili.
Juu ya mikanganyiko
iliyojitokeza Oseah amesema Simba imewasilisha fomu mama na mkataba wa mlinzi
wake wa zamani Kelvin Yondani bila ya kuambatanisha fomu ya usajili ya mlinzi
huyo ambapo kwa ujumla Simba imewasilisha jumla ya majina ya wachezaji 28.
Kwa upande
wa klabu ya Yanga ambayo ilimtumia mlinzi Yondani katika michuano ya Kombe la
Kagame wamewasilisha kila kitu ikiwemo fomu mama, fomu ya usajili wake pamoja na
mkataba wa mlinzi huyo aliyehamia klabu hiyo kwa mbinde toka Simba na
wakiorodhesha jumla ya majina ya wachezaji 28.
Wakati hayo
yakiwa hivyo nayo Azam fc imewasilisha tff jina la kiungo Ramadhani Chombo
Lidondo pamoja na mkataba wake ndani ya klabu hiyo ilhali Simba wakiwasilisha
vielelezo vyote muhimu ikiwemo fomu mama, fomu ya usajili na mkataba wake ndani
ya klabu hiyo msimu huu.
Kwa upande
wa ligi daraja la kwanza ni vilabu vitano tu vilivyowasilisha majina ya usajili
wao wa wachezaji kati ya vilabu 24.
Katibu huyo
wa tff Oseah amesema kwasasa inasubiriwa kamati ya Katiba,sheria na hadhi ya
wachezaji chini ya mwenyekiti wake Alex Mgongolwa kuketi na kuamua juu ya hayo
kwa kuwa kanuni ziko kimya juu ya hayo.
SIKILIZA HAPA.
Kuna matatizo sana pale TFF.Vilabu vya Simba na Yanga wanapewa inside information na TFF offices na cha ajabu hakuna anayehoji kuwa ni vipi Simba au Yanga wawe na informanation za ndani za mchezaji wa timu nyingne?Hatuwezi kufika hata siku moja.
ReplyDelete