Koffi
Olomide, ambaye ni mwanamuziki mashuhuri barani Afrika ameshitakiwa kwa kumpiga
Mtayarishaji wake wa muziki.
Mwanamuziki
huyo alikamatwa na kufungiwa katika kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani
jumatano.
Taarifa
zinazohusianaAfrika, drc
Koffi alikamatwa
kufuatia vurugu katika hoteli moja mjini Kinshasa.
Waandishi wa
habari wanasema mahakama hiyo ya Kinishasa ilifurika kutokana na watu wengi
kuja kumuona kiongozi huyo wa bendi ya Quartier Latin akiwa kizimbani.
Kesi hiyo
iliharishwa hadi Alhamisi asubuhi wakati atakaposhitakiwa rasmi.
Wakati wa
kesi hiyo hapo jana Koffi Olomide aliwakilishwa na mawakili 10.
Ugomvi kati
ya mwanamuziki huyo na mtayarishi wake Bwana , Diego Lubaki, ni kuhusu pesa
dola $3,680.
Hakimu
alimfahamisha mwanamuziki huyo ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela
miezi sita.
Olomide ni
gwiji wa muziki aina ya "soukous", mtindo ulitokana na jina la
kifaransa "secouer", lenye maana ya kujitikisa au kujinengua ,na
wachezaji wake vile vile wanatambulika kwa kunengua maungo.
No comments:
Post a Comment