Adebayor anategemea mambo mazuri na Tottenham msimu huu
Mshambuliaji
wa Tottenham Emmanuel Adebayor ametanabaisha kuwa anategemea kuwepo katika
kipindi kizuri cha kudumu katika klabu yake hiyo baada ya mpango wa kudumu
kukamilika.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 28 amefanikiwa kupata mkataba wa kudumu kwa gharama
ya pauni milioni £5 toka Manchester City wiki hii na anamatumaini ya kujenga zaidi
uwezo wake wa kufumania nyavu zaidi ya magoli 18 aliyofunga msimu uliopita pale
White Hart Lane.
Adebayor alikuwa
ni sehemu muhimu katika kikosi cha Harry Redknapp ambacho ilikuwa kidogo
kucheza vilabu bingwa Ulaya kutokana na Chelsea kutwaa taji la Ulaya mwezi May.
Amenukuliwa Adebayor
akisema,
"mwaka
uliopita nilikuwa katika kipindi kigumu , na hiyo ndio sababu kila mchezo msimu
huu utakuwa mgumu kama ulivyoona mchezo wa jumamosi. Newcastle walikuwa na timu
nzuri.
"Manchester
United, Manchester City, Chelsea, Arsenal, Tottenham na Newcastle watakuwa
katika vita ya kuwania nafasi za juu nne.
"haitakuwa
rahisi, lakini kama mcheza soka unapaswa kufanya mambo yako na kuangalia nini
kimetokea mwisho wa msimu."
Mambo ya
kifedha yalimchelewesha Adebayor kupata mkataba wa kudumu kule kaskazini mwa London
toka Manchester City na mshambuliaji huyo raia wa Togo amefurahia kupata
mkataba huo.
Leonardo:Messi & Cristiano
Ronaldo si lolote si chochote kwa Ibrahimovic.
Mkurugenzi wa
soka wa Paris Saint-Germain Leonardo anadhani hakutakuwa na mshambuliaji bora
kuliko Zlatan Ibrahimovic, na kusisitiza kuwa MSwedish huyo hawezi
kulinganishwa na Lionel Messi au Cristiano Ronaldo.
amenukuliwa
na L’Equipe Leornado akisema
"tunaweza
kuwazungumzia Messi na Cristiano Ronaldo, lakini si lolote kwa Ibrahimovic. kwa kilo 100 na mita 1.96 ni bora katika kufumania nyavu duniani ,"
"wakati
tunamsaini Thiago Silva na Zlatan msimu
huu kila mtu alivutiwa na kile tulicho kifanya baada ya miaka miwili au mitatu watu
watakuwa na majibu sahihi juu ya utoufauti tunaousema"
Mbrazil huyo
amesisitiza kuwa wameweka offer nyingine kwa ajili ya mlinzi wa Lille ya
Ufaransa Mathieu Debuchy.
amesema,
"ni
mchezaji mkubwa na ni mchezaji wa wakala huyo huyo wa Mathieu Bodmer,kwa hiyo
unaweza kusema kuwa tumesha kuwa karibu naye. hatukuwahi huko nyuma kuzungumzia
hili .."
PSG imekuwa
katika jitihada ya kutafuta kiwango bora katika wiki za mwanzo wa kununua
wachezaji msimu huu lakini Leonardo amekuwa hana mashaka juu ya zoezi hilo.
Paris
Saint-Germain inatarajia kufungua msimu mpya wa ligi ya Ufaransa “Ligue 1” kwa
ngarambe itakayopigwa pigwa jumapili dhidi ya Bordeaux.
Giggs: usajili wa RVP ni ujumbe
Usajili wa Manchester United kwa Robin van
Persie toka Arsenal ni ujumbe mkubwa kuwa klabu hiyo inataka kuchukua mataji msimu
huu, hii ikiwa ni kauli ya mkongwe Ryan
Giggs.
Van Persie alijunga
na Old Trafford toka Emirates kwa ada ya pauni milioni £24 baada ya msimu wa
tetesi kubwa kuwa alikuwa na mpango wa kuaelekea katika vilabu kadhaa ikiwepo Manchester
City na Juventus.
Mkongwe
Giggs anasema United ilikuwa imejipanga kufunika machungu yake ya kukosa taji
msimu uliopita kwa utofauti wa mabao ya kufunga na kufungwa na kumaliza msimu
uliopita mikono mitupu nyuma ya City.
amenukuliwa
Giggs kupitia mtandao wa United akisema
"Usajili
wa Van Persie ni ujumbe mkubwa, ni jambo kubwa kwa mchezaji kuja hapa na kusema
alikuwa anataka kuja katika klabu hii.
"Najipendelea
lakini wachezaji wanapaswa kuwa na utashi wa kuja United kwasababu tuna kawaida
ya kuwa na “guaranteed” ya kutwaa mataji
hiyo ndiyo ‘spirit’ yetu na unapata nafasi ya kufundishwa na meneja mkubwa . kuna
mengi yakujivunia."
Thomas
Muller haoni sababu kwa nini mbio za taji la soka nchini Ujerumani isiwe ya
vilabu Bayern Munich na Borussia Dortmund.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Ujerumani anadhani timu nyingine zinaweza kuingia katika
mbio hizo za taji tangu mapema kwa msimu lakini akaongeza kuwa ni BVB na Bayern
zinazoweza kuwa katika changamoto ya taji mpaka kumalizika kwa msimu.
amenukuwa
kupitia mtandao wa klabu akisema
"unaweza
kuziona timu nyingine nyingi katika mbio lakini kimsingi nadhani Bayern na Dortmund
ni timu mbili zenye ubora na uwezo katika kipindi chote ".
Mshambuliaji
huyo mwenye uwezo mkubwa pia amezungumzia juu ya mchezo wa ufunguzi mwishoni
mwa juma wa ligi kuu ya nchini Ujerumani Bundesliga dhidi ya Greuther Furth
akisema timu hiyo mpya haita kuwa daraja.
"utakuwa
ni mchezo mgumu ,Furth iko katika kiwango kizuri hasa baada ya kupata nafasi ya
kujiweka vizuri kimaandalizi na wanaweza wakaendeleza historia yao nzuri ya
kufanya vizuri katika uwanja wao wa nyumbani,".
Stramaccioni amwagia sifa kwa Zaneti akimuita 'bionic'
Kocha wa Inter
Milan Andrea Stramaccioni amesema nahodha wake Javier Zanetti ni sawa na "bionic"
yaani kifaa ambacho kinamsaidia mwanadamu kufanya kazi kuwa rahisi wakati huu
ambapo mchezaji huyo akiwa katika maandalizi ya kukamilisha mchezo wake wa 800th
ndani ya klabu hiyo hii leo.
Stramaccioni
amenukuliwa akisema Zanetti ambaye
kwasasa ana umri wa miaka 39, "is not human".
Ametoa kauli
hiyo kwa waandishi wa habari kuelekea kwenye mchezo wa kuwanuia kufuzu michuano
ya Europa League dhidi ya Vaslui ya Romania.
Kioungo huyo
raia wa Argentina alijiunga na Inter mwaka 1995,na kukamilisha jumla ya michezo
700 katika mchezo wa fainali ya Ligi ya mabingwa mwaka 2010 mchezo ambao Inter Milan
iliichapa Bayern Munich mabao 2-0 kule Bernabeu.
Stramaccioni
ambaye kiumri ni mdogo kwa utofauti wa miaka mitatu amenukuliwa akisema
"ni
kitu cha kipekee . sikuwahi kufikiri au
kuona mtu anacheza michezo 800 katika maisha yangu yote . nahodha wangu lazima
atakuwa ‘cloned’ yaani mtu wa tofauti ."
Zanetti pia
anashikilia rekodi ya kucheza michezo mingi katika timu ya taifa ya Argentina akicheza
michezo 145 na kucheza michezo zaidi ya 1,000 katika career hii.
No comments:
Post a Comment