Mourinho:Goli la kwanza la Barcelona la off-side.
Jose Mourinho na Tito Vilanova wakipeana mikono baada ya mchezo kumalizika |
Kocha wa Real
Madrid Jose Mourinho anaamini kuwa mwamuzi wa pembeni alifanya kosa kubwa kwa
kuruhusu goli la Pedro na kupelekea mchezo kumalizika kwa matokeo ya timu yake
kuchapwa mabao 3-2 na Barcelona katika
mchezo wa kwanza wa Supercopa.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Hispania alifunga goli la kusawazisha la Barca kunako
dakika ya 56 baada ya baada ya kumzidi Fabio Coentrao, lakini kupitia luninga
ilionekana kuwa alikuwa tayari amejenga kibanda yaani ameotea.
Amenukuliwa
Mourinho akisema
“goli la
kwanza la Barcelona lilikuwa ni makosa ya mwamuzi na ndivyo ilivyo,”
Kocha huyo
raia wa Ureno ameelezea juu ya uwezo wa kikosi chake ikiwa ni pamoja na
kumpongeza winga wake Jose Callejon.
“si kupenda
kipindi cha kwanza kilivyokuwa lakini katika kipindi cha pili mambo yalikuwa
tofauti. Callejon alicheza vizuri. Alimuandalia mazingira mazuri kimchezo Di
Maria. Huu uilikuwa ni mchezo muhimu nimependa kazi yakek,”
Katika
mchezo wa pili Supercopa itahamia Santiago Bernabeu baada ya siku sita, lakini
pia timu zote hizo zitakuwa katika michezo ya ligi ya Hispania La Liga mwishoni
mwa juma ambapo Madrid watakuwa na kibarua dhidi ya Getafe na Barcelona dhidi
ya Osasuna.
Marcelo: Supercopa ni kama imekwisha
Marcelo |
Mlinzi wa
kushoto wa kimataifa wa Brazil na Real Madrid Marcelo anaamini taji la
Supercopa litakwenda Bernabeu lakini pia akifurahishwa na mchezo ulioonyeshwa
na Madrid dhidi ya Barcelona.
Akiongea na TVE
baada ya mchezo huo Clasico uliomalizika kwa Madrid kuchapwa mabao 3-2 kule Camp
Nou,mlinzi huyo wa pembeni amefarijika na kiwango cha Los Blancos na anaamini kikosi chake kinafaida
ya kufanya vizuri zaidi katika mchezo wa wa marudiano.
Alexandre Song-Nataka kushinda mataji na
Barcelona
Kiungo mpya
wa Barcelona Alexandre Song amesema anatamani kutwaa mataji na kufanya vizuri
akiwa ndani ya jezi ya blaugrana baada ya kusaini katika klabu hiyo kwa mkataba
wa miaka mitano akitokea Arsenal.
Akiongea kupitia
mtandao wa klabu yake amesema anajisikia fahari kuwa ni sehemu ya kikosi cha Tito
Vilanova ambacho kinacheza 'tiki-taka'
style.
Kiungo huyo
wa kimataifa wa ambaye anacheza kama kiungo mkabaji ameweka wazi matarajio yake
kuwa atakuwa kwenye kipindi cha mafanikio chini ya kocha wake mpya Vilanova.
Song ambaye
amekabidhiwa jezi nambari No. 25 amemzungumzia
rafiki yake wa karibu toka wakiwa wote Arsenal Cesc Fabregas kuwa ndiye chagizo la
kumfanya acheze mpira mzuri Camp Nou.
Song anaamini
kuwa atafanikiwa kuhimili kipindi hiki kigumu cha mpito cha kutoka kwenye soka
la English mpaka Hispania na anadhani uwezo wake na fitness yake itajihirisha
kuwa ni azina kubwa ndani ya Camp Nou.
"niko
vizuri katika mazingira ya mtu na mtu kwa kawaida huwa najaribu kuupata mpira. Nafikiri
mpira wa kingereza na Hispania kuna tofauti kidogo. Uingereza ni nguvu kidogo
tofauti na hapa hivyo napaswa kuiga. Sidhani kama aina yangu ya mchezo
itabadilika lakini nitalazimika kuwa vizuri zaidi”
No comments:
Post a Comment