BOBAN |
KIUNGO mshambuliaji wa Simba,
Haruna Moshi 'Boban' na beki wa kati wa timu hiyo, Juma Nyosso wametemwa katika
kikosi cha timu hiyo.
Boban ameshindwa kwenda mkoani
Tanga, ambako kesho watacheza na Mgambo
Shooting, kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, kutokana na kukabiliwa na maumivu
ya misuli.
Timu hiyo iliyoondoka Dar es
Salaam jana, ikiwa na wachezaji 24, Nyosso alimeondolewa katika kikosi
kitakachocheza kesho kutokana na anakadi tatu za njao.
Ofisa Habari wa Klabu
hiyo, Ezekiel Kamwaga alisema leo kuwa
wachezaji waliobaki Dar es Salaam
ni Shomari Kapombe, Haruna Shamte na Kigi Makasi ambao ni majeruhi.
Wachezaji waliondoka
ni Juma Kaseja, Wilbert Mweta, Waziri Hamad, Nassor Masoud 'Chollo', Amir Maftah, Paulo Ngalema,
Koman Bili Keita, Pascal Ochieng, Hassan
Kondo na Jonas Mkude.
Wengine ni Ramadhani
Chombo 'Redondo', Amri Kiemba, Abdallah Seseme, Ramadhani Singano, Uhuru
Selemani, Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto, Salim
Kinje, Abdallah Juma, Daniel Akuffo, Felix Sunzu, Edward Christopher,
Haruna Athumani na Emmanuel Okwi
Wakati huo huo, Kocha wa timu
hiyo, Milovan Cirkovic amesema baada ya kupoteza pointi sita kutokana na
kutoka sare katika mechi tatu kikosi chake kipo fiti katika mchezo huo.
Cirkovic alisema matokeo hayo ya
sare hayamaanishi timu yake ni mbovu ila mashabiki wanatakiwa kuondoa wasiwasi
juu ya kiwango cha timu yao.
Alisema kupoteza pointi sita sio
tatizo ila ni matokeo ya mchezo, kwani
hakuna timu inayokwenda uwanjani kwa lengo la
kufungwa.
Wakati huo huo, Uongozi wa klabu hiyo imesema unatarajia kuliweka kitimota benchi
la ufundi kutokana na mwenendo wa timu hiyo kutoka sare mfululizo.
Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Geofrey Ngange
'Kaburu' alisema kutokana na ushindani wa ligi hiyo, matokeo hayo ni mabaya kwa
upande wao kwani wanatakiwa kushinda la sio kutoka sare.
Kaburu alisema baada ya kushindwa kuifunga Coastal
Union na Kagera Sugar, wanaelekaza nguvu katika mchezo wa Jumapili dhidi ya
Mgambo ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi
pole kamanda
ReplyDelete