Aliyekuwa mgombea wa DRFA Amin Bakhiressa |
KAMATI
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imechukua uamuzi magumu,
baada ya kumwengua Mwenyekiki wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA),
Amin Mohamed Bakhresa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu wa chama hicho.
Bakhressa
ambaye alikuwa madarakani zaidi ya miaka 10 hatima yake ya kuendelea kuwania tena ndani ya chama hicho
ilifikia tamati leo, baada ya kubainika hana sifa inayostahili kwa mujibu wa
katiba ya DRFA.
Uchaguzi
huo ambao ulipangwa kufanyika Oktoba 14, umesongezwa mbele hadi Desemba 8,
mwaka huu, baada ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA iliyochini ya Mwenyekiti wake,
Muhindin Ndolanga kufutwa.
Kamati
hiyo ilihusika kwa kiwango kikubwa katika ukiukwaji wa kanuni na taratibu za
uchaguzi na kutozingatia matakwa ya katiba ya DRFA katika mchakato wa uchaguzi
wa viongozi wa chama hicho.
Akizungumza
Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Deogratias Lyatto,
alisema kwa kuzingatia katiba ya TFF, ibara ya 40(1), kanuni za uchaguzi za
wanachama wa TFF ibara ya 10(6), 12(1) na 26(2)na (3), imeifuta kamati ya DRFA.
Lyatto
alisema DRFA imeagizwa kuteuwa kamati mpya ya uchaguzi itakayoandaa na kutekeleza
majukumu yake ikizingatia Kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF na Katiba ya
DRFA.
Alisema
uteuzi huo unatakiwa kufanyika kabla ya Oktoba 25 mwaka huu, ambapo mchakato wa
uchaguzi utaanza upya utaanza Oktoba 29 mwaka huu.
Hata
hivyo, Lyatto alisema kamati yake ilipitia rufani mbalimbali zilizowasilishwa na
vyama vya soka vya Mkoa wa Mbeya, Shinyanga na Dar es Salaam.
Kamati
hiyo ilipokea rufaa dhidi ya Mohamed Salim Bakhressa, ambaye aliomba kuwania nafasi
ya mwenyekiti wa DRFA iliyowakilishwa na ichael Wambura na
Juma Jabir iliomba
jina liondolewa katika orodha ya wagombea kwa kuwa hana elimu ya kiwango cha
kidato cha nne na hivyo kutokidhi matakwa ya Katiba ya DRFA Ibara ya 29(2).
‘Mtu yeyote anayegombea nafasi yoyote ya
DRFA hana budi awe na kiwango cha elimu kisichopungua kidato cha nne,"
alisema Lyatto.
Lyatto
alisema baada ya kupitia vielelezo kuhusu rufaa dhidi ya maamuzi ya kamati ya
uchaguzi ya DRFA na kujadili maelezo ya warufani, Kamati ya Uchaguzi ya DRFA na ilijiridhisha Bakhressa hana elimu ya kiwango hicho.
Alisema
kwa kutokidhi matakwa hayo ya katiba ya
DRFA, hastahili kugombea nafasi ya mwenyekiti wa DRFA na kamati ya uchaguzi
ilikubaliana na maombi ya warufaa.
Kamati ya uchaguzi ya DRFA iliwapitisha
wagombea Gungurugwa Tambaza, Mohammed
Bhinda, Benny Kisaka na Hamisi Ayoub 'Mpapai' bila kuwa na vielelezo
vinavyothibitisha kuwa wana kiwango cha elimu kisichopungua kidato cha nne.
Kutokana na mkanganyiko, maelezo yenye utata
kutoka kwa warufani na warufaniwa na maamuzi ya utata ya kamati ya uchaguzi ya
DRFA, yameufanya mchakato wa uchaguzi wa DRFA, kupoteza hadhi ya uchaguzi
unaozingatia Kanuni za uchaguzi na misingi ya demokrasia na uwazi kama
ilivyoainishwa kwenye kanuni za uchaguzi za TFF.
No comments:
Post a Comment