Katibu mkuu wa TFF Angetile Oseah. |
Pia
Kamati ilijadili mchakato wa chaguzi za Chama cha Madaktari wa Michezo
(TASMA) na kupokea mchakato wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa wa
Mbeya (MRFA).
Baada ya kujadili chaguzi hizo kwa kina, Kamati ilifikia uamuzi ufuatao:
1. FRAT
Uchaguzi
wa FRAT haukufanyika baada ya wajumbe kugoma wakipinga kuondolewa kwa
baadhi ya wagombea. Kamati ilikubaliana kuiagiza Kamati ya Uchaguzi ya
FRAT kuhakikisha uchaguzi unafanyika Novemba 17, 2012 na kufanya
maandalizi yote muhimu ikiwa ni pamoja na sehemu ambako uchaguzi huo
utafanyika. Mkutano utatakiwa kuwapigia kura wajumbe waliopitishwa
kugombea uongozi tu.
2. RUREFA
Baada
ya kufuta uchaguzi wa viongozi wa RUREFA na kuivunja Kamati ya Uchaguzi
ya RUREFA, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitaka Kamati ya Utendaji ya
RUREFA kuteua kamati mpya ya uchaguzi ya chama hicho kabla ya Oktoba 20,
2012 na kuiagiza kamati mpya kuwa imeshatangaza mchakato wa uchaguzi
ifikapo Oktoba 24, 2012.
3. SHIREFA
Kamati
ilipokea pingamizi dhidi ya baadhi ya wagombea uongozi wa SHIREFA na
hivyo kuagiza walioweka pingamizi na waliowekewa pingamizi pamoja na
mwakilishi wa Kamati ya Uchaguzi ya SHIREFA kuhudhuria kikao cha Kamati
ya Uchaguzi ya TFF kitakachofanyika Alhamisi ya Oktoba 18, 2012 kwa
ajili ya maamuzi ya mwisho.
4. MRFA
Kamati
ilipokea rufaa na pingamizi kutoka kwa baadhi ya wagombea walioenguliwa
kuwania uongozi wa chama hicho na hivyo imewataka walioweka pingamizi
na waliokata rufaa kuhudhuria kikao cha Kamati ya Uchaguzi ya TFF
kitakachofanyika Oktoba 18, 2012 jijini Dar es salaam.
5. TASMA
Kamati
iliona mapungufu katika mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa TASMA na
kuamua chama hicho kifanye uchaguzi ifikapo Desemba mosi badala ya
uchaguzi kufanyika Oktoba 27, 2012 kama
ilivyokuwa imepangwa awali. Kamati ya Uchaguzi ya TFF inaiagiza Kamati
ya Uchaguzi ya TASMA kuhakikisha kasoro zilizojitokeza zinarekebishwa
ili uchaguzi ufanyike kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho na Kanuni za
Uchaguzi.
6. DRFA
Awali,
Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilitangaza kuwa hatma ya uchaguzi wa DRFA
itajulikana baada ya kikao cha leo, lakini kutokana na wajumbe kutoweza
kuhudhuria kwa sababu tofauti, mustakabali wa suala hilo sasa
utajulikana baada ya kikao cha Oktoba 18, 2012.
Wagombea
na wadau wanaotakiwa kuhudhuria kikao cha Oktoba 18, 2012 wanataarifiwa
kuwa kikao hicho kitafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za TFF
kuanzia saa 08:2012.
Kamati inawaomba wajumbe wote kuhudhuria bila ya kukosa.
Angetile Osiah
Katibu Mkuu TFF
No comments:
Post a Comment