MASHINDANO YA MITUMBWI YA BALIMI EXTRA LAGER 2012, MOTO KUANZIA KIGOMA.
|
Meneja wa Bia ya
Balimi Extra Lager Edith Bebwa akiwa na Meneja Masoko wa Tbl Fimbo
Buttala kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia
bia yake ya Balimi Extra Lager leo imezindua rasmi mashindano ya
mitumbwi kwa kanda ya ziwa mwaka 2012. Mashindano
hayo ya kupiga kasia, yanayo dhaminiwa na bia ya “Balimi Extra Lager”
yatashirikisha mikoa ya Kigoma, Kagera, Mwanza, Mara na visiwa vya
Ukerewe. Mashindano haya yamekuwa yakijizolea umaarufu katika kanda ya
ziwa mwaka hadi mwaka na yametokea kuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa
Kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kufuatia mashabiki na wapenzi wa mchezo
huo kuongezeka kila mwaka. Akiongelea
mashindano ya mwaka huu wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Balimi
Extra Lager Edith Bebwa alisema, Ni zaidi ya miaka saba sasa, bia ya
Balimi imekuwa ikiendesha mashindano haya katika kanda ya Ziwa na mkoani
Kigoma, kwa kipindi chote hiki Balimi imefanikiwa kuleta changamoto
kubwa katika mchezo wa kupiga makasia, kwa kuwapa fursa wapiga makasia
kutumia mitumbwi yao katika michezo na kujipatia kipato cha ziada
kupitia zawadi nono zinazotolewa lakini pia kuleta burudani kwa wakazi
wanaozunguka ziwa Victoria na lile la Tanganyika.
Kwa
hivi sasa timu zote zimeshaanza maandalizi, tayari kwa mashindano ya
ngazi ya mkoa ambapo kwa mwaka huu yataanzia Kigoma tarehe 20 Octoba,
ikifuatiwa na Kagera tarehe 27 Octoba, Mwanza tarehe 4 Novemba, Kisiwa
cha Ukerewe tarehe 10 Novemba na Mara tarehe 17 Novemba. Baada ya
fainali hizo za ngazi ya mikoa timu zilizoshinda zitakutana katika
fainali kuu itakayofanyika Jijini Mwanza tarehe 2 Desemba pale Mwaloni
Kirumba.
Akizungumzia
timu zitakazofuzu kuingia fainali kuu, Bi Edith alisema; timu tatu za
wanaume na mbili za wanawake zitakazoshika nafasi za juu zaidi katika
ngazi ya mkoa ndizo zitakazoingia katika fainali kuu itakayofanyika
Jijini Mwanza.
Na
timu zilizochukuwa ubingwa mwaka jana upande wa wanaume na wanawake
watapata fursa ya moja kwa moja ya kuingia finali kuu za mwaka huu ili
kutetea ubingwa wao.
Akizitaja
zawadi watakazopata washindi katika ngazi za Mkoa na fainali kuu,
Meneja Masoko Bw. Fimbo Butallah alisema; Kama ilivyo ada, zawadi
zimekuwa zikiongezeka kila mwaka, ukiwemo mwaka huu 2012 |
No comments:
Post a Comment