Mmiliki wa Liverpool
Fenway Sports Group amethibitisha kujipanga kwa ajili ya kuendeleza dimba la Anfield.
Malumbano baina
ya klabu hiyo na halmashauri ya mji wa Liverpool juu ya kubomoa nyumba za
karibu na uwanja huo yanaonekana kufikia ukingoni licha ya matangazo ya ukarabati
wa kuongeza uwezo wake wa watazamaji kuelezwa kuwa utafanyika baadaye.
Mkurugenzi wa
klabu hiyo Ian Ayre ametanabaisha kuwa Liverpool imekuwa kifanya kazi bega kwa began
a mamlaka ya mji huo ili kufikia makubaliano ambayo yataendeleza eneo lote linalo
zunguka Anfield.
Amenukuliwa
mkurugenzi huyo akisema
"ujenzi
mpya wa Anfield ni kitu ambacho wakaazi na watu wengi mji mzima wamekuwa
wakizungumza na wote tumegundua kuwa klabu ya soka ni mwajiri, ni biashara na
pia ni mkazi wa eneo hili."
Ayre, pia
amezungumzia juu ya kuendelea kuwepo hapo kwa klabu hiyo huku akidai kuwa
kujenga uwanja mpya ni jambo la gharama.
Cazorla: najaribu kumuiga Iniesta wa Barcelon
Santi
Cazorla amesema nyota Andres Iniesta ambaye ni mchezaji anaye tokea katika
taifa moja la Hispania , amesema kuwa mchezaji wa kuigwa na yeye amekuwa kwenye
ndoto ya kufikia uwezo wa kiungo huyo.
Cazorla anacheza
msimu wake wa kwanza katika ligi kuu ya nchini England na amekuwa akivutia
katika uchezaji wake ikiwa ni pamoja na kutoa pasi za mwisho na hata kufunga
katika michezo saba ya msimu huu akiwa na Arsenal.
Lakini nyota
huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye ametokea Malaga katika kipindi cha uhamisho
wa kiangazi anaamini Iniesta ni mchezaji ambaye kila mtu anapenda kumuangalia.
"Iniesta
ni kiwango ambacho mimi nachukulia kama kipimo changu. Kucheza kama yeye ni
kitu kingine. Ni mcheza soaka aliyekamilika katika kila kitu"
"najaribu
kuiga kila kitu anachofanya lakini ni ngumu sana. Tatizo ni kwamba anapokuwa
anafanya jambo unaliona kama rahisi lakini unapokwenda kujaribu unakutana na
ugumu. Andres ni ‘role model’ wangu ndani na nje ya uwanja."
No comments:
Post a Comment