SIMBA YAANZIA RAUNDI YA NANE KWA KAGERA SUGAR
Ligi
Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi nane
kesho (Oktoba 17 mwaka huu) kwa mechi tano huku vinara wa ligi hiyo
Simba wakiialika Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Mechi
hiyo namba 52 itachezeshwa na mwamuzi Ronald Swai kutoka Arusha wakati
waamuzi wasaidizi ni Julius Kasitu na Methusela Musebula, wote kutoka
Shinyanga. Mwamuzi wa akiba ni Ephrony Ndisa wa Dar es Salaam huku
mtathimini wa waamuzi akiwa Charles Mchau kutoka Moshi.
Uwanja
wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya
Tanzania Prisons inayofundishwa na Jumanne Chale na Azam iliyo chini ya
kocha Boris Bunjak kutoka Serbia. Nayo Polisi Morogoro iliyopanda msimu
huu itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Mgambo
Shooting ambayo imepata ushindi mara mbili mfululizo itakuwa nyumbani
Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga ikiikaribisha Toto Africans katika
mechi itakayochezeshwa na Geofrey Tumaini wa Dar es Salaam. Oljoro JKT
inayonolewa na Mbwana Makata itakuwa nyumbani Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha dhidi ya African Lyon.
No comments:
Post a Comment