Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ambaye
ndiye Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo tayari ametoa notisi
ya mkutano huo utakaofanyika Februari 23 na 24 mwakani jijini Dar es
Salaam.
Mkutano
huo utafanyika Februari 23 mwakani na kufuatiwa na ajenda ya uchaguzi
siku inayofuata. Ajenda ya uchaguzi iko chini ya Kamati ya Uchaguzi ya
TFF.
Notisi
hiyo imetumwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ambao ni kutoka vyama vya
mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki, klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na
wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF.
Ajenda za Mkutano Mkuu zitatumwa kwa wajumbe siku 15 kabla ya mkutano huo wenye wajumbe zaidi ya 100.
NUSU FAINALI UHAI CUP KUPIGWA KARUME
Mechi
za nusu fainali ya michuano ya Kombe la Uhai 2012 inayoshirikisha timu
za vijana wenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom
zitachezwa kesho (Desemba 21 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume, Dar es Salaam.
Nusu
fainali ya kwanza ya michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Said
Salim Bakhresa kupitia maji Uhai itazikutanisha timu za Mtibwa Sugar ya
Morogoro na Azam na itafanyika kuanzia saa 2 kamili asubuhi.
Simba
na Coastal Union zitacheza nusu fainali ya pili kuanzia saa 10 kamili
jioni kwenye uwanja huo huo. Mtibwa Sugar imepata tiketi ya nusu fainali
baada ya kuichapa African Lyon mabao 3-1 wakati Simba iliilaza Oljoro
JKT mabao 2-0.
Nayo
Azam iliindoa JKT Ruvu kwenye robo fainali kwa bao 1-0 huku Coastal
Union ikipata ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mechi
ya mwisho ya robo fainali.
Mechi
ya fainali na ile ya kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa Jumapili
(Desemba 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es
Salaam. Mechi ya mshindi wa tatu itaanza saa 2 kamili asubuhi wakati ya
fainali itakuwa saa 10 kamili jioni.
PONGEZI KWA UONGOZI MPYA TWFA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaupongeza uongozi mpya wa Chama cha
Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) uliochaguliwa katika
uchaguzi uliofanyika jana (Desemba 19 mwaka huu) hoteli ya Midlands
mjini Morogoro.
Ushindi
aliopata Lina Kessy aliyechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti pamoja na
wajumbe wengine wa Kamati ya Utendaji unaonesha jinsi ambavyo wajumbe wa
Mkutano Mkuu wa TWFA walivyo na imani kwao.
TFF
inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya TWFA, na
kwamba ina changamoto kubwa ya kuhakikisha inaendesha shughuli za chama
hicho kwa kuzingatia katiba na kanuni.
Pia
tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA chini ya Mama Ombeni
Zavala na Kamati ya Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Deogratias Lyatto
kwa kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa utulivu na kwa kuzingatia
Katiba ya TWFA na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Safu
mpya ya uongozi wa DRFA inaundwa na Lina Kessy (Mwenyekiti), Rose
Kissiwa (Makamu Mwenyekiti), Amina Karuma (Katibu), Zena Chande
(Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa TFF) wakati mjumbe wa Kamati ya Utendaji
ni Triphonia Temba.
No comments:
Post a Comment