Mwakilishi wa Tanzania ni Joceline Diana Maro (miaka 220 |
|
Guetano
Kagwa ambaye anatarajiwa kuwa MCwa shindano hilo akizungumza na waandishi wa habari
katika mkutano huo uliofanyika jana jijini Dar es salaam, kulia ni Rena
Calist Mkurugenzi wa Miss East Africa.
Warembo wanaoshiriki katika shindano hilo wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo jana.
.
Baadhi ya
washiriki wa shindano hilo ni pamoja Jocelyne Diana Maro (22yrs) kutoka
Tanzania,Elidas Ella Chirwa (22yrs)kutoka Malawi,Rahwa Afeworki (22yrs) kutoka
Eritrea, Akuot Philip Suzan (20yrs) kutoka Sudan.
Wengine ni Ayisha
Nagudi (23yrs) kutoka Uganda, Annabelle Marvel Pointe (19yrs)kutona Seychelles
na Lula Teklehaimanot (19yrs) kutoka Ethiopia .
Taji la Miss
East Africa linaloshikiliwa na mrembo kutoka Rwanda, Cyntia Akazuba, ndiye
atakayemvika taji mshindi atakayetwaa taji hilo hii leo Ijumaa.
Mshindi wa
kwanza atapata jumla ya dola za Kimarekani 30,000 pamoja na gari aina ya Mazda
lenye thamani ya dola 15,000 na mkataba wa kufanya kazi na Oganaizesheni ya
Miss East Africa wenye thamani ya dola 15,000.
Mshindi wa
pili atapata zawadi zenye thamani ya dola 8,000 ikiwa ni pamoja na kitita cha
dola 2,000 na mkataba wa kufanya kazi na Oganaizesheni ya Miss East Africa
wenye thamani ya dola 6,000.
Mshindi wa tatu
atapata zawadi zenye thamani ya dola 5,000 pamoja na fedha taslimu dola 1,500
na mkataba wa kufanya na Oganazesheni ya Miss East Africa wenye thamani ya dola
3,500.
Shindano
hili la kimataifa linashirikisha warembo kutoka nchi za Tanzania (mwenyeji),
Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia,
Malawi, Seychelles na South Sudan; na warembo mbalimbali wa Afrika Mashariki
walioshindana katika nchi mbalimbali za Ulaya ambazo ni Ubelgiji, Ufaransa na
Uholanzi.
No comments:
Post a Comment