KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, January 14, 2013

MOURINHO ALIKUWA OLD TRAFORD KUCHUNGUZA MBINU ZA MZEE FURGERSON


Meneja wa Real Madrid Jose Mourinho jana alikuwa ni miongoni mwa watazamaji walikuwa uwanjani Old Traford wakishuhudia pambano la mahasimu wa soka nchini England baina ya Manchester United dhidi ya Liverpool wakati huu linasubiriwa pambano baina ya timu yake na United mwezi ujao.

Mourinho na meneja wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola ni miongoni mwa makocha wakubwa wenye majina barani Ulaya ambao wanatarajiwa kuhudhuria seminar ya makocha barani ulaya kupitia chama chao cha mameneja wa ligi kuu (League Managers' Association (LMA).

Hata hivyo wadau wa soka nchini England wameitafsiri hiyo kama ni mbinu mbadala ya Mourinho kuichunguza United huku yeye na Guardiola wakihusishwa kuchukua nafasi ya kumrithi Sir Alex Ferguson katika viunga vya Old Trafford wakati utakapofika kwa mskochi kuyo kujiuzulu.

Pia meneja wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson naye alikuwepo jukwaani akiangalia viwango vya wachezaji wake Michael Carrick, Steven Gerrard, Tom Cleverley na wengine wakati huu ambapo England inajiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Brazil mwezi ujao.
Mchezo huo ulimazika kwa united kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1 mabao ya United yakifungwa na Van Persie na Vidic na bao la Liverpool likifungwa na Danniel Sturridge.
Pichani juu Jose Mourinyo akifuatilia pambano la watani United na Liverpool.
Roy Hogdson naye alikuwepo akiwakagua wachezaji wake wa timu ya taifa.
Van persie anatupia bao la kwanza.
Danniel Sturrigde naye anafunga bao pekee la Liverpool.
Nimanja Vidic anafunga bao la pili la United.

No comments:

Post a Comment