KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, January 13, 2013

UKURASA WA HABARI ZA KIMATAIFA: Mzee Wenger anasema Fabregas anaweza kurudi Arsenal. Fabio Capello kuhudhuria sherehe za miaka 150 za England FA na O'Brien aongeza mkataba West Ham.

 Wenger: Fabregas anaweza kurudi Arsenal.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema upo uwezekano mkubwa wa kiungo wake wa zamani Cesc Fabregas kurejea Emirates Stadium.
Fabregas mwenye umri wa miaka 25, aliichezea kwa miaka minane Arsenal kabla ya kurejea nyumbani Hispania katika klabu iliyomkuza tangu akiwa mtoto ya Barcelona kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 30 mwaka 2011.
Wenger anaamini kuwa kiungo huyo wa kimataifa ya Hispania kwasasa ametulia Camp Nou, na timu yake ikiongoza ligi ya nchi hiyo Liga lakini bado anaamini anaweza kurejea kusaini tena Arsenal.
"Sidhani kama hararejea moja kwa moja iko siku moja " amekaririwa na gazeti la Guardian.
"ni mtu wa Arsenal. Anaipenda Arsenal na anaangalia kila mchezo wa Arsenal. Lakini bila shaka Barcelona kulikuwa ndiyo nyumbani alikokulia lazima ukubali hilo.
"Huenda asije mwakani au miaka miwili au mitatu kwasababu ana uhusiano mkubwa na Barcelona. Lakini baadaye linawezekana."
Wenger kwasasa amepata faraja kubwa kwa wachezaji wake vijana waingereza Kieran Gibbs, Carl Jenkinson, Jack Wilshere, Aaron Ramsey na Alex Oxlade-Chamberlain – kusaini mkataba mpya na klabu hiyo.


Capello kuhudhuria sherehe za FA.
 Meneja wa zamani wa timu ya taifa ya England Fabio Capello atakuwa ni miongoni mwa watu watakao hudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 150 ya chama cha soka cha England jumatano jijini London.
Sherehe hizo ambazo pia zitahudhuriwa na meneja wa sasa wa England na zitafanyika Connaught Rooms huko Holborn.
Kwasasa Capello ni meneja wa timu ya taifa ya Russia, na tayari ameuarifu uongozi wa FA ataudhuria katika sherehe hizo.
Capello aliondoka kuifundisha England kwa mizengwe mwezi February 2012 baada ya kutofautiana na maamuzi ya kumvua unahodha John Terry kwa mara ya pili na tangu wakati huo hakuwa na mawasiliano na FA.
Ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 150 ya FA, pia kumeandaliwa michezo miwili ya kirafiki kati ya England na Brazil na mchezo mchezo mwingine kati ya Scotland dhidi ya jamhuri ya Ireland. Michezo mingine dhidi ya Ujerumani na Argentina inatarajiwa kuchezwa baadaye mwaka huu.

O'Brien asaini new West Ham.
 Mlinzi wa West Ham Joey O'Brien ameongeza mkataba mwingine na klabu hiyo ambao utamuweka klabuni hapo mpaka 2016.
O'Brien akiwa chini ya Sam Allardyce katika klabu ya Bolton alipelekwa Upton Park mwaka 2011 na bosi wa washika nyundo.
Klabu hiyo imetangaza hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa maneno yaliyosomeka “West Ham United inayofuraha kubwa kutangaza kuwa Joey O'Brien amesaini mkataba mpya utakamuweka klabu mpaka kiangazi 2016.”
O'Brien mwenye umri wa miaka 26, ameitumikia timu ya taifa ya jamhuri ya Ireland michezo mitano na ameitumikia klabu yake michezo 16 huu wa ligi kuu ya England ‘Premier League’ akifunga magoli mawili.

No comments:

Post a Comment