KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, February 11, 2013

Azam FC na Yanga alama sawa tofauti magoli, yaichapa Mtibwa Sugar 4-1 kwao Manungu Complex.

Maandalizi mazuri, uwekezaji mkubwa wa miundombinu na utaalam na usajili mzuri yameipatia Azam FC ushindi mnono kwa kuifunga Mtibwa Sugar 4-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliochezwa kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Ushindi huo wa ugenini umeiongezea Azam FC pointi tatu na kufikisha jumla ya pointi 33 ikiwa sawa na Yanga wakitofautiana kwa magoli, na Simba kuwa ya tatu ikiwa na pointi 27.
Katika mchezo huo ujio mpya wa mchezaji Kipre Tchetche pamoja na kandanda safi lililochezwa na Azam FC limeipatia ushindi timu hiyo na kuongeza rekodi ya kuifunga timu Mtibwa kwa mara ya nne ikiwa katika uwanja wa nyumbani kwao Manungu.
Azam FC walianza mchezo huo wakijiamini na mapema katika dakika ya 14 mchezaji Jockins Atudo aliipatia Azam FC goli la kwanza akimalizia krosi iliyopigwa na Abdi Kassim ‘Babi’.
Dakika ya 21 Vincent Barnabas akaisawazishia Mtibwa Sugar kwa mpira wa kichwa baada ya kuteleza kwa kipa Mwadini Ally wakati akitaka kudaka mpira aliorudishiwa kwa kichwa na beki Jockins Atudo, timu zikaenda mapumziko zikiwa sare ya 1-1.
Kipindi cha pili kilikuwa cha Azam FC, walipata goli la pili dakika 47 lililofungwa na mshambuliaji Brian Umony aliyecheza vizuri na Humphrey Mieno na kuwapoteza mabeki wa Mtibwa na kuandika goli hilo ambalo lilibadili matokeo yakawa 2-1.
Azam FC walifanya mabadiliko dk 45 alitoka Himid Mao akaingia Ibrahim Mwaipopo alieyefanya kazi nzuri kipindi cha kwanza, dk 60 Abdi Kassim alipumzishwa baada ya kuitendea haki safu yake ya ushambiliaj nafasi yake ikachukuliwa na Tchetche Kipre na dk 75 alitoka Brian Umony aliyefunga goli la pili akaingia kiungo Jabir Aziz.
Mabadiliko hayo yaliimarisha kikosi cha Azam FC na kuzidi kuitesa Mtibwa Sugar ambao walionekana kupata tabu, dk 88 Kipre Tchetche aliipatia Azam FC goli la tatu kwa shuti akimalizia mpira aliotengewa na Humphrey Mieno na kupeleka matokeo kuwa 3-1.
Mshambuliaji huyo (Kipre) kutoka Ivory Coast alitumia vizuri dakika za nyongeza kwa kuipatia Azam FC goli la nne na kuhitimisha kalamu ya magoli baada ya kuunganisha vizuri mpira uliopigwa na nahodha Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na kumaliza mchezo Azam FC ikiondoka na ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji wao Mtibwa Sugar.
Azam FC ilianza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam mara baada ya mchezo huo kwa ajili ya kuanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza wa kimataifa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Nasri Juba ya Sudan Kusini utakaochezwa wiki ijayo jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Azam FC kilichofanya mauaji kiliundwa na Mwadini Ally, Himid Mao/Ibrahim Mwaipopo 45’, Malika Ndeule, Jockins Atudo, David Mwantika, Michael Bolou, Brian Umony/Jabir Aziz 75’, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (cpt), Abdi Kassim ‘Babi’/Tchetche Kipre 60’ Humprey Mieno na Khamis Mcha

No comments:

Post a Comment