KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, February 11, 2013

NIGERIA BINGWA MARA TATU AFRIKA. WAICHAPA BUKINA FASO 1-0 JOHANESBURG. STEPHEEN KESHI ANASTAHILI PONGEZI.

Cup of joy: A jubilant Nigeria squad hoist the Africa Cup of Nations trophy aloft for the third time
Shangwe na furaha: wachezaji wa Nigeria wakinyanyua juu kombe la ubingwa ikiwa ni mara ya tatu kulinyakua katika historia ya fainali hizo.Always in control: Sunday Mba flicked the ball over a defender with his right, before firing home the only goal of the final with his other foot
Nigeria imefanikiwa kuchukua kwa mara ya tatu taji la soka la mataifa ya Afrika baada ya kuifunga Bukina Faso bao 1-0 huku Nigeria ikitawala mchezo wa fainali uliopigwa jijini Johannesburg.
Sunday Mba aliifungia Nigeria maarufu kama 'Super Eagles' bao hilo zuri kwa mpira wa kubetua na kuusukumiza wavuni mpira wa kunyunyiza 'volley' zikiwa zimesalia dakika tano kabla ya mapumziko baada ya muda mrefu wa kutafutana kwa tahadhari kubwa, huku pongezi kubwa zikimuangukia kocha mzalendo na nahodha wa zamani wa timu hiyo Stephen Keshi.
Always in control: Sunday Mba flicked the ball over a defender with his right, before firing home the only goal of the final with his other foot
Sunday Mba akijaribu kuubetua mpira juu ya mlinzi wa Bukina Faso kabla ya kuusukumiza wavuni na kuwa goli pekee lililo ipa ushindi Nigeria. Picha ya chini Mba na wachezaji wengine wa Nigeria wakishangilia baada ya goli kuingia.
Winner: Sunday Mba is congratulated by Nigeria team-mates after firing the only goal of the game
Hiyo ilikuwa ni fainali ya kwanza kwa Nigeria tangu mwaka 2000 lakini pia walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo tangu mapema kufuatia rikodi yao ya kucheza michezo 12 bila ya kufungwa.
Fancy seeing you again: Nigeria coach Stephen Keshi grabs the Africa Cup of Nations trophy after winning the competition as a player in 1994
Kocha wa Nigeria Stephen Keshi akishilia kombe la ubingwa kwa furaha akikumbuka alipolinyakuwa kombe hilo kama mchezaji mwaka 1994.
Safe hands? Vincent Enyeama clings on despite pressure from Prejuce Nakoulma
Vincent Enyeama akipaa angani kuunyakuwa mpira licha ya kukabiliwa na Prejuce Nakoulma.

Baada ya Nigeria kufanikiwa kutwaa taji hilo, mantiki yake ni kuwa kocha Keshi anakuwa kocha wa pili kushinda taji hilo akiwa mchezaji na pia kama kocha akifuata nyayo za Mahmoud Al Gohari wa Misri.
No holds barred: Burkina Faso's Mady Panandetiguiri clashes with Nigeria keeper Vincent Enyeama
Mlinda mlango wa Nigeria Vinvent Enyeama akikabiliana na  Mady Panandetiguiri.
Outnumbered: Nigeria's Victor Moses scraps for possession with Burkina Faso's Bakary Kone (centre), Mohamed Koffi (back) and Djakaridja Kone (right)
Victor Moses wa Nigeria akijaribu kuuwahi mpira huku akipata upinzani kutoka kwa Bakary Kone wa Bukina Faso(katikati), Mohamed Koffi (nyuma) na Djakaridja Kone (kulia).

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Burkina Faso kufikia fainali ya michuano hiyo ambapo mwaka 1998 walifanikiwa kutinga hatua ya nufu fainali ambapo walipoteza mchezo huo kwa waliokuwa mabingwa Misri.
Pamoja na kufungwa lakini walionyesha uwezo ambapo katika sehemu ya kiungo Jonathan Pitroipa alionyesha ubunifu mkubwa na kutawala sehemu hiyo.
Itakumbukwa Pitroipa ndiye aliyepewa kadi nyekundu kimakosa katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ghana.
At full stretch: Burkina Faso keeper Daouda Diakite repels a Nigeria attack
Mlinda mlango wa Burkina Faso Daouda Diakite akizuia hatari kutoka kwa washambuliaji wa Nigeria.
Holding on: Burkina Faso keeper Diakite saves from MosesWarm welcome: FIFA president Sepp Blatter was made to feel at home in Johannesburg
Rais wa FIFA Sepp Blatter alikuwepo uwanjani.
Warm welcome: FIFA president Sepp Blatter was made to feel at home in South Africa

No comments:

Post a Comment