Amir Khan (kulia) akimchakaza Carlos Molina. |
Amir Khan anatarajiwa kucheza kwa mara ya kwanza katika ardhi ya nyumbani nchini Uingereza baada ya miaka miwili kupita baada ya kuthibitishwa kuwa bondia huyo wa uzito wa light-welterweight atacheza dhidi ya Julio Diaz mwezi Aprili.
Bingwa huyo wa zamani wa dunia atakuwa akikutana na bondia Diaz raia wa Mexico huko Sheffield Aprili
27 likiwa ni pambano lake la kwanza katika ardhi ya Uingereza tangu apate ushindi ulioibua gumzo kubwa dhidi ya Paul McCloskey mwaka 2011.
Pambano la mwisho la Khan lilikuwa ni dhidi ya Carlos Molina jijini Los Angeles mwezi Desemba mwaka jana likiwa ni pambano lake la ushindi baada ya kupoteza mfululizo mapambano yake mawili dhidi ya Lamont Peterson na Danny Garcia.
Khan atakuwa akirejea Uingereza kwa lengo la kujijenga upya ambapo atakuwa akicheza katika ukumbi wa Motorpoints Arena ambao una uwezo wa kuchukua watazamaji 12,000.
Hata hivyo inavyoonekana haitakuwa kazi nyepesi kwa Khan kushinda kutokana na rekodi nzuri ya bondia wa Mexico Diaz ya kushinda mapambano 40 kwenda sare mapambano 7 na kupigwa pambano moja (40-7-1) ambapo katika mapambano aliyoshinda kuna mapambano 29 ameshindwa kwa KO.
Khan akicheza pambano lake la mwisho nchini Uingerza dhidi ya Paul McCloskey (kulia).
No comments:
Post a Comment