Mshambuliaji wa Yanga Jerrison Tegete akiambaa na mpira baada ya kumtoka mlinzi wa Kagera Sugar. |
Wachezaji wa Yanga wakitoka uwanjani mara baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar kumalizika. |
Ligi kuu ya soka Tanzania bara imeendelea tena hii leo ambapo vinara wa msimamo wa ligi hiyo Yanga walikuwa dimbani wakicheza dhidi ya Kagera Sugar mchezo uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Yanga imefanikiwa kuendeleza furaha ya ushindi kwa mashabiki wake baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lilifungwa na kiungo hodari Haruna Niyonzima.
Niyonzima alifunga bao hilo kunako dakika ya 65 ya mchezo baada ya kupokea pasi ya mlinzi wa pembeni Oscar Joshua.
Pengine Yanga wangeibuka na ushindi mnene zaidi ya huo wa mabao 2 kufuatia mshambuliaji wake Didier Kavumbagu kuangushwa katika eneo la hatari na mlinda mlango wa Kagera Sugar Hannington Kalyesubula kunako dakika ya 45 ya mchezo lakini penati iliyopigwa na Kavumbagu mwenyewe kushindwa kutinga wavuni na kupaa juu ya lango la Kagera sugar.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuzidi kujikita kileleni katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa sasa imefikisha jumla ya alama 42 zaidi ya alama 6 za Azam fc wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na alama 36.
No comments:
Post a Comment