KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, February 25, 2013

SIMBA YATAFUNISHWA MIWA NA MTIBWA BILA YA KUPENDA.

Bingwa mtetezi wa taji la ligi kuu ya soka Tanzania bara Simba ameendelea kujiweka katika nafasi mbaya zaidi ya kutetea taji lake, kufuatia kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka wageni Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani Morogoro katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Bao pekee la washindi lilifungwa na Salvatory Enterbe kunako dakika ya 19 ya mchezo ambaye alipanda mbele kushambulia ambapo aliunasa mpira wa pasi ya mwisho ya Vicent Barnabas baada ya kuwalamba chenga walinzi wawili wa Simba katika eneo la hatari la lango la Simba kabla ya Enterbe kuachia shuti la chini chini na kupita kushoto kwa mlinda mlango Juma Kaseja
.
Matokeo hayo yameifanya Simba kusalia na alama 31 baada ya kucheza michezo 18 ya ligi hiyo huku Mtibwa wakifikisha alama 27 na kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi. 
 
Kwao Simba ambao walianza vizuri msimu huu wa ligi na hata wakati fulani kuongoza ligi kwa tofauti kubwa ya alama dhidi ya mtani wao Yanga ambao ndio vinara wa msimamo kwasasa, itabidi wajiulize sana wapi walipokwama mpaka kufikia kutokupata matokeo mazuri uwanjani.

Kwasasa hali imeshaanza kuwa ngumu kwa upande wa uongozi wa juu wa klabu hiyo ambapo viongozi wao wamekuwa wakilazimika kuondoka uwanjani mapema kabla ya mchezo kumalizika na kuwaacha mashabiki wakisalia uwanjani kwa muda mrefu wasijue nini cha kufanya baada ya mchezo  mpaka wanatawanywa na jeshi la Polisi linalo tishia kutumia kurusha maji ya kuwasha.

No comments:

Post a Comment