Mlinda mlango wa Everton Tim Howard atalazimika kuwa pembeni
ya uwanja kutokana na kuthibika kuwa mlinda huyo amevunjika mfupa wa mgongo.
Mlinda mlango huyo raia wa marekani mwenye umri wa miaka 34
amepatwa na dhahma hiyo katika mchezo wa marudiano wa michuano ya FA mzunguko wa tano dhidi ya Oldham siku 11
ziliaopita
Meneja wake David Moyes anadhani Howard huenda akaendelea kuwepo nje ya uwanja
kwa wiki nne.
Mlinda mlango wa kimataifa wa Slovakia Jan Mucha, ambaye
alianza kuichezea timu hiyo wiki iliyopita katika mchezo dhidi ya Reading,
ataendelea kuwepo katika goli la timu hiyo katika mchezo wa robo fainali ya
dhidi ya Wigan hii leo.
Licha ya kumbwela msimu, wakala wa Samir Nasri anasema ataendelea kumpigania city.
Wakala wa Samir Nasri
amesisitiza kuwa atahakikisha anapigania hatma ya baadaye ya nyota ndani
ya Manchester City.
Nyota huyo wa kimataifa wa ufaransa mwenye umri wa miaka 25 amekuwa mbali na mafanikio yake msimu huu akiwa pia ameanza katika kikosi cha kwanza nusu tu ya michezo ya ligi ya Manchester City
Nasri amekuwa akikosolewa waziwazi na meneja wake Roberto
Mancini kutoka na kiwango chake cha msimu huu, hali ambayo imekuja baada ya
kampeni ngumu ya Euro 2012 ambapo Nasri alizozana na mwandishi wa habari na
kupelekea kufungiwa na michezo mitatu na shirikisho la soka la nchi yake ya
Ufaransa FFF.
Licha ya yote hayo kumkumba Nasri, bado wakala wake Jean-Pierre
Bernes anadhani mshambuliaji huyo atarejea katika hali yake ya kawaida.
No comments:
Post a Comment