Mashabiki wa soka wa klabu ya Al-Ahly katika jiji la Cairo nchini Misri wamezua balaa katika jiji hilo ikiwa ni pamoja na kuichoma moto ofisi ya shirikisho la soka nchini humo kufuatia mahakama jijini Cairo kutoa hukumu ya kifo kwa mashabi 21 wa soka.
Mapema asubuhi ya leo mahakama ya Cairo imethibitisha hukumu ya vifo hivyo kufuatia kuuwawa kwa mashabiki 74 na wengine zaidi ya 1,000 kujeruhiwa baada ya mchezo uliopigwa mwezi januari baina ya Al Masri ya Port Side na Al-Ahly.
Hukumu ya kifo iliyotolewa mwezi Januari imethibitishwa hii leo na mahakama mjini Cairo na kupokelewa kwa hasira nchini humo.
Wale waliohukumiwa kifo wengi wao ni mashabiki wa Al Masry ya Port Said ambao buila shaka sasa watakuwa wanaelekea kunyongwa.
Vurugu kubwa zimeibuka katika mji wa Suez Canal city.
Itakumbukwa watu 40 walifariki dunia mara baada ya hukumu hiyo kutangazwa kwa mara ya kwanza January 26, na wengi wao waliuwawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Itakumbukwa watu 40 walifariki dunia mara baada ya hukumu hiyo kutangazwa kwa mara ya kwanza January 26, na wengi wao waliuwawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Mashabiki
wengi wa Al Masry katika mji wa Port Said, wanadhani kuwa mamlaka
imeipendelea klabu ya Al-Ahly, kwa kuwa ni klabu kubwa nchini Misri.
Filimbi
ya mwisho ilipo pulizwa katika mchezo baina ya Al-Masry na Al-Ahly
February 1 mwaka jana ulipelekea kuzuka kwa vurugu kubwa na watu 130,000
kujeruhiwa vibaya na vitu vyenye ncha kali kama visu, vyuma, kuwasha
moto pamoja kuwavamia wachezaji wa Al-Ahly na mashabiki wao karibu.
Hasira kutoka kwa mashabiki wa Al-Ahly wakionyesha hasira zao.
Moshi mkubwa ukitoka kutoka katika ofisi za shirikisho la soka la nchini Misri
Fans protesting
wapingaji wa hukumu iliyotolewa katika mji wa Port Said katika picha hii leo.
Watu wamekusanyika kusikiliza hukumu.
No comments:
Post a Comment