Rafael Benitez ashinda zawadi ya meneja bora wa mwezi April ligi ya Premier. |
Bosi wa Chelsea Benitez ametangazwa kuwa meneja bora wa mwezi wa April licha ya kuwa ni meneja wa muda wa klabu ya Chelsea.
Bosi huyo wa Chelsea ametangzwa kuwa bora kufuatia kucheza michezo minne ndani ya mwezi huyo bila ya kupoteza mchezo hata mmoja na hivyo kuweka vizuri matumaini ya Chelsea kupata nafasi moja kati ya nne za juu mwishoni kwa msimu.
Heshima hiyo ya mwezi inafuatia pia muda mfupi baada ya bosi wa Manchester United Alex
Ferguson kusema kuwa amekuwa akivutiwa na CV nzuri ya meneja huyo anayoitengeneza ndani ya Stamford Bridge akiwa meneja.
Kwa mara ya mwisho Chelsea kutoa meneja bora wa mwezi ilikuwa ni mwezi April 2011, kabla ya kufukuzwa kwa Carlo Ancelotti.
Lkini hata hivyo licha ya kuzongwa na ukosoaji kutoka kwa mashabiki wa Cheslea Benitez amerejesha heshima kwa kutengeneza mazingira mazuri ya klabu hiyo kumaliza ligi ikiwa katika nafasi ya tatu na pia kutinga fainali ya michuano ya vilabu ya Europa League.
Ferguson
alikaririwa Ijumaa iliyopita akisema
'Ki ukweli kabisa kwake amefanya kazi nzuri ndani ya wiki chache zilizopita na hiyo imemjengea CV. '
Ferguson pia ameshawahi kushinda zawadi ya meneja wa mwezi ndani ya msimu huu.
Benitez ameshinda zawadi hiyo mara sita ndani ya career yake.
Possibility: Many Chelsea fans may take issue with this sign.
No comments:
Post a Comment