Oscar akiwa na wachezaji wenzake wa Chelsea wakielekea uwanja wa ndege kutokea katika uwanaja wao mazoezi wa Cobham. |
Chelsea hii leo imesafiri kuelekea Amsterdam kwa ajili ya mchezo wa fainali ya michuano ya Europa ikiwa ni kampeni yao ya pili kusaka taji la vilabu barani Ulaya baada ya miaka mingi.
Chelsea watakuwa wakipambana na Benfica katika dimba la Amsterdam ArenA hapo kesho katika usiku wa fainali Europa na hii leo asubuhi meneja wa muda kla kikosi hicho Rafa Benitez aliambatana na wachezaji wake kutoka katika uwanja wa mazoezi wa Cobham na kuelekea uwanja wa ndege.
Benfica
watakuwa wakiingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kichapo kutoka kwa wapinzani wao wakubwa katika kusaka taji la ligi kuu ya Ureno Porto mchezo uliopigwa mwisho wa wiki iliyopita kikiwa ni ichapo cha kwanza katika msimu wa ligi ya nchi hiyo.
Nahodha wa Chelsea John Terry, mshambuliani Eden
Hazard na kiungo John Obi Mikel pia wameelekea Amsterdam licha ya wasiwasi juu ya afya zao.
Kikosi cha Chelsea kikipanda basi na kuanza safari ya kuelekea Amsterdam kuivaa Benfica katika fainali ya Europa hapo kesho.
Terry anakabiliwa na matatizo ya kifundo cha mguu ilhali Hazard anasumbuliwa na msuli maumivu aliyoyapata katika mchezo wa jumamosi iliyopita wa ligi kuu ya England dhidi ya Aston Villa.
Terry hakuwepo katika fainali ya msimu uliopita ya ligi ya mabingwa mjini Munich kutokana na kusimama kwa adhabu kadi na hivyo maumivu aliyonayo sasa yana maanisha kuwa huenda akakutana na kuikosa kwa mara nyingine tena fainali hiyo muhimu barani Ulaya.
Nahodha huyo wa zamani wa England mwenye umri wa miaka 32 na kuiweka Chelsea katika wakati mgumu wa kusaka mbadala wake baina ya David Luiz, Gary Cahill na Branislav Ivanovic.
Juan Mata akipanda basi.
Frank Lampard ambaye alitengeneza rekodi ya mfungaji wa kihistoria wa Chelsea katika mchezo uliofanyika Villa Park, huenda akapangwa katika kiungo kuziba nafasi ya Obi Mikael akisaidiana na Luiz na Ramires katika kusukuma mashambulizi sambamba na Juan Mata na Oscar.
Ryan Bertrand atakuwa akichukua nafasi ya Ashley Cole katika sehemu ya ulinzi wa kushoto kufuatia kuonyesha kandanda safi katika mchezo fainali mjini Munich miezi 12 iliyopita.
Kiungo Oriol Romeu, ambaye hakuwepo dimbani kufuatia maumivu ya mguu pia amesafiri pamoja na mduchi mwenye umri mdogo wa miaka 18 Nathan Ake.
Yupo pia mshambuliaji Demba Ba licha ya kwamba hatakuwepo kikosini kwani alikuwa akitumiwa na Newcastle mapema katika michuano hii hivyo amepoteza uhalali.
Mlinzi David Luiz
Kukosa uhalali kwa Ba ni wazi kwamba Fernando
Torres ataanzishwa kikosini sehemu ya ushambuliaji licha ya kwamba mshambuliaji huyo amekuwa si lolote si chochote katika msimu huu licha ingawa alisajiliwa na mapesa mengi .
Chelsea imeondoka na walinda mlango wanne Petr
Cech, Ross Turnbull, Hilario na Jamal Blackman na mlinzi wa kireno Paulo Ferreira licha ya kwamba hatachezeshwa katika mchezo huo dhidi ya ndugu zake wa Ureno.
Eden Hazard amesafiri licha ya kuwa mgonjwa.
Mata
John Terry na Frank Lampard.
Oscar
Rafa Benitez
Lampard na Petr Cech
Mshabikiwa kwa Benfica wakiwa wamejianda kwa kushangilia huko Dam Square.
Amsterdam Arena
Meneja wa Benfica Jorge Jesus akishuka uwanja wa ndege wa Holland tayari kwa mchezo hapo kesho.
.
Mlinzi wa Benfica Luisao.
Oscar Cardozo na Lorenzo Melgarejo wanamatumaini ya kuizamisha Chelsea.
Ashley Cole na Gary Cahill wakiwasili hotelini Asterdam.
No comments:
Post a Comment