Imefahamika Kuwa
Roberto Mancini alifukuzwa kuwa meneja wa Manchester City kutokana na
mawasiliana na mabaya baina yake na matendaji.
Kushindwa
kwake kuendeleza wachezaji vijana ilikuwa pia ni sababu ya kuondolewa kwake
kibaruani.
City
inafikiria kumchukua kocha wa Malaga Manuel Pellegrini licha ya kwamba mpango
huo kuonekana haujakamilika bado
Kwasasa meneja
msaidizi Brian Kidd atakuwa kibaruani kwa muda kama meneja wa kikosi hicho.
Atakuwepo katika
benchi la ufundi katika michezo miwili ya mwisho ya ligi dhidi ya Reading hii
leo na mchezo mwingine dhidi ya Norwich Jumapili pamoja na michezo ya safarini
nchini Marekani mwishoni mwa mwezi huu wa May wakati huu City ikisaka mbadala
wa Mancini.
David Beckham kusalia Paris St-Germain
Paris
St-Germain wanataka kusalia na David Beckham msimu ujao hata kama asipokuwa
mchezaji.
Beckham
mwenye umri wa miaka 38, aliingizwa katika mchezo wa Jumapili baina ya PSG na Lyon ambao PSG
ilichomoza na ushindi wa bao 1-0 .
Akiongea na
L’Equipe Rai wa klabu hiyop Nesser Al-Khalaii amesema
"Ameamua
kuchana kucheza soka lakini nina matumaini atasalia kwa kazi nyingine," .
Alipoulizwa
juu ya nini mipango yake kiungo huyo wa zamani wa England amesema
"Niko
katika furaha usiku huu hilo ndilo la msingi"
PSG inaamini
kumpatia Beckham mkataba mwingine wa miezi mitano kama alivyofanya wakati
akijunga nayo mwezi Januari baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka sita katika
klabu ya Los Angeles Galaxy ya nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment