Akijadili mipango yao ya baadaye Lampard akiwa na mchumba wake ambaye ni mtangazaji wa TV Christine Bleakley. |
Frank Lampard sasa amepata ahueni ama nafuu juu ya kikwazo cha maamuzi yake ya kutaka kujunga na LA Galaxy kufuatia kushaurina na mchumba wake Christine Bleakley kwa lengo la kuungana naye nchini Marekani.
Mkataba wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 na klabu yake ya sasa ya Chelsea unamalizika mwishoni mwa msimu huu ambapo maamuzi ya kujiunga na ligi ya Marekani MLS yanabaki wa kwa kiungo kama ataondoka Stamford Bridge majira ya kiangazi yajayo.
Huko nyuma mchumba wake alionyesha kutokuwa tayari kuelekea Los Angeles na kama alivyonukuliwa mwezi Januari alisema,
‘Mimi ni ndege wa nyumbani, kuja London ilikuwa ndio mpango kwangu.
‘I’m as far away from my mum and sister now than I feel comfortable with.’
Lakini hata hivyo kwasasa inavyoonekana ni kwamba mtangazaji huyo wa TV ameanza kuonyesha dalili za kubadili mawazo yake na kuanza kuwa tayari kutaka kuelekea LA should Lampard seal his move to the Home Depot Center.
Kwasasa kinachoonekana ni kwamba wanajipanga na maisha mapya wakijadiliana kuhusu mali na eneo la kuanzisha maisha hayo mapya nchini Marekani ili kuhakikisha kuwa kuhama kwao na kuvuka bahari ya Atlantic
kunakwenda salama.
Hata hivyo kulikuwepo na taarifa mwezi February juu ya Chelsea kutaka kubadili mawazo yao ya awali ya kutaka kubakisha tena kiungo huyo na kwamba mazungumzo huenda yakafanyika juu ya kumuongezea mkataba mwingine.
Inavyoonekan ni kwamba kwa meneja yoyote mpya atakaye ajiriwa Chelsea atataka kuendelea kusalia na mfungaji huyo wa pili katika historia ya klabu hiyo msimu ujao.
Lampard yuko goli moja nyuma ya Bobby Tambling anashikilia rekodi ya ufungaji mabao mengi ya Chelsea.
Lampard ameifungia Chelsea jumla ya mabao 201. |
Lampard
ameifungia Chelsea jumla ya mabao 201. Kiungo huyo ana michezo sita ndani ya msimu ya kumuwezesha kufunga na kuifikia rekodi hiyo ya Tambling ambapo Chelsea wana mchezo wa kivumbi cha michuano ya Europa mchezo wa marudiano dhidi ya Basle mchezo utakapigwa Stamford Bridge.
Meneja wa muda Rafa Benitez anaendelea kupata shinikizo la kutakiwa kumtumia Lampard ili afikishe na kuvunja rekodi ya mabao ya klabu hiyo ambapo katika siku za hivi karibuni meneja huyo amekuwa akimtumia kama mchezaji wa akiba.
No comments:
Post a Comment