Manuel Charr (kulia) mwenye matarajio ya kumchapa mpinzani wake David Haye(kushoto) |
David Haye amesisitiza kumchapa mpinzani wake Manuel Charr, licha ya kwamba alikuwa nje ya ulingo kwa akaribu mwaka mzima.
Pambano hilo litakalo pigwa katika ukumbi wa Manchester Arena June 29 litashuhudia bingwa wa zamani wa uzito wa juu wa mkanda wa WBA Haye akicheza kwa mara ya kwanza tangu amchape mwingireza mwenzake Dereck Chisora mjini in London mwezi Julai mwaka 2012.
Charr mwenye umri wa miaka 28, ndani ya kipindi hicho ameshapigana mara tatu akipigwa na bingwa wa WBC Vitali Klitschko kabla ya kurejea katika ushindi mara mbili na kutengeneza rekodi ya kushinda mapambano 23 na kupoteza moja.
Haye mwenye rekodi ya kushinda 26 na kupigwa 2, ambaye anarejea baada ya kumchapa Chisora, hana wasiwasi na kazi yake ambapo amesisitiza kuwa yuko tayari kwa ajili ya Charr.
Akimzungumzia Charr mjini Manchester hapo jana katika mkutano na waandishi wa habari , Haye amesema
'Yuko thabiti na ngangari na ana moyo akilisubiri pambano hilo'.
Toe-to-toe: Majigambo.
Charr ana kila kitu kudhihirisha kuwa yuko sawa dhidi ya Haye mjini Manchester June 29
Respect: Haye anaamini atakuwa katika hali nzuri na kumchapa mzaliwa wa Lebanon.
No comments:
Post a Comment