John Terry hayuko salama Chelsea, anasema
Jose Mourinho
Meneja wa Chelsea
Jose Mourinho amesisitiza kuwa nahodha wkae John Terry hayuko sawa na kwamba
atatakiwa kudhihirisha ubora wake katika kikosi cha kwanza ndani ya mkataba
wake.
Terry mwenye
umri wa miaka 32 alikuwa ni skipper muhimu
katika kikosi cha Mourinho kuanzia mwaka 2004 mpaka 2007 na kwasasa amesaliwa
na mwaka mmoja ndani ya mkataba wake.
Mourinho amesema
"Hayuko sawa na mwenyewe anajua kuwa
hayukoa sawa. Kitu pekee anachojua ni juu ya urafiki wake lakini kiutaalamu hakuna
aliye sawa.
Terry
akitwaa mataji chini ya Mourinho
Premier League (2): 2004-05, 2005-06
FA Cup (1): 2006-07
Football League Cup (2): 2004-05, 2006-07
FA Community Shield (1): 2005
Zambia yashinda taji la Cosafa Cup
Zambia imetawazwa
ubingwa wa michuano ya COSAFA kwa mara ya nne baada ya kufanikiwa kuwachapa
walikuwa mabingwa watetezi wa taji hilo Zimbabwe kwa mabao 2-0 katika mchezo wa
fainali ya michuano hiyo uliopigwa katika uwanja wa Ndola.
Magoli mawili
kila kipindi yalifungwa na Alex N'gonga na Kabaso Chongo yaliibeba Zambia waliokuwa
wenyeji wa michuano hiyo.
Chipolopolo waliaanza
kupata bao la kwanza dakika ya tano kufuatia mpira wa N'gonga wa free kick kuwapita
walinzai wa Zimbabwe maarufu kama Brave Warriors.
Bao la pili
lilifungwa katika dakika ya mwisho kufuatia mpira wa moja kwa moja wa adhabu wa
Chongo kwenda moja kwa moja ndani ya nyavu.
Zimbabwe ilipata
nafasi kadhaa za kufunga katika lango la wapinzani wao lakini walishindwa
kuupeleka mpira nyavuni huku mlinda mlango wa Zambian Danny Munyau kusimama
imara.
Pepe Reina wa Liverpool kujiunga na Napoli kwa mkopo
Mlinda mlango
wa Liverpool Pepe Reina anajipanga kujiunga na Napoli kwa mkopo wa muda mrefu.
Kocha wa Napoli
Rafael Benitez amekuwa akimkufukuzia Mhispania mwenzake huyo ambaye alikuwa
nambari moja kipindi chake Anfield, baada ya kushindwa kumnasa mlinda mlango wa
QPR Julio Cesar.
Reina mwenye
umri wa miaka 30, alitarajiwa kurejea mazoezini katika klabu yake Jumapili kwa
kujiunga na wachezaji wenzake huko katika ziara ya maandalizi ya msimu.
Liverpool ilimsainisha
mlinda mlango raia wa Belgium Simon Mignolet kutoka katika klabu ya Sunderland kwa
ada ya uhamisho ya pauni milioni £9 mwezi uliopita.
Reina alijunga
na Liverpool akitokea Villarreal mwaka 2005.
Flamengo ya Brazil yamsajili kwa mkataba wa kudumu mlinzi wa Arsenal Andre Santos.
Arsenal imemuuza
mlinzi wake wa kushoto Andre Santos katika klabu ya Flamengo ya nchini Brazil.
Mlinzi huyo
mwenye umri wa miaka 30 alijung a Gunners akitokea Fenerbahce ya Uturuki kwa ada ya wakati huo ya pauni
milioni £6.2 mwezi August 2011 lakini alishindwa kuonyesha ubora wa soka yake
ndani ya klabu hiyo
Andre Santos
at Arsenal
Appearances:
33
Goals (all
competitions): 3
Alirejea katika
taifa lake la Brazil na kujiunga na Gremio kwa mkopo mwezi January 2013 kufuatia
Arsenal kumsajili mlinzi mwingine wa kushoto Nacho Monreal kutoka katika klabu
ya Malaga.
Santos
ambaye alikuwa kwa mkopo katika klabu ya Flamengo katika msimu wa 2005-06 sasa
anajiunga nao tena kwa mkataba wa kudumu.
Taarifa ya
klabu ya Arsenal kwa njia ya mtandao imearifu kuwa "Kila mtu ndani ya Arsenal
angependa kumshukuru Andre kwa mchango wake ndani ya klabu na anamtakia kila la
kheri huko baadaye"
Ameichezea Arsenal
michezo 33 na kuifungia mabao matatu .
No comments:
Post a Comment