Papiss Cisse agomea kuvaalia nembo ya mdhamini wa klabu yake Wonga na aachana na safari ya Ureno na timu yake ya Newcastle.
Mshambuliaji wa Newcastle United Papiss Cisse
ameshindwa kusafiri na klabu yake katika ziara ya maandalizi ya kuanza msimu nchini Ureno kama kielelezo cha kugomea vifaa vya mazoezi vyenye nembo ya wadhamini wa klabu hiyo Wonga.
Wonga ni moja ya taasisi za kifedha nchini England inayotoza riba kubwa ya ukopaji kwa mteja wake ambayo imeingia mkataba wa udhamini na klabu hiyo ya Newcastle United wa miaka minne mkataba ambao uliingiwa mwaka jana.
Mshambuliaji huyo raia wa Senegal kwasasa anafanya mazoezi yake binafsi baada ya kurejea kutoka katika mapumziko ya kumalizika msimu baada ya kugomea kuvalia vifaa vyeneye nembo ya Wonga kutokana na nembo hiyo kwenda kinyume na imani yake ya dini ya kiislamu.
Mchezaji huyo na klabu yake walikuwa katika majadiliano makali juu ya suala hilo ikiwa ni pamoja na kuitwa katika chama cha wachezaji wa kulipwa PFA, ambapo ilidhaniwa angesafiri kuelekea Ureno ambako Newcastle itakuwa huko kwa wiki nzima ambapo itacheza michezo miwili dhidi ya Rio Ave na Pacos Ferrerira.
Hapo jana Jumanne usiku baada ya mchezo wa kufungua msimu katika maandalizi ya klabu hiyo ambapo walichomoza na ushindi dhidi ya Motherwell huko Scotland, Pardew alitangaza kuwa atakuwa akisafiri na kikosi chake kizima kuelekea Ureno ikiwa ni pamoja na Cisse.
Lakini mshambuliaji huyo hakuonekana katika ndege iliyoondoka uwanja wa ndege wa Newcastle hii leo mchana na tetesi zinasema huenda alilazimishwa kuondoka St James’s Park.
Cisse
alijunga na Newcastle akitokea Freiburg kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £9 mwezi Januari mwaka jana na alikuwa katika msimu mzuri akiwa ndani ya jezi nambari 9 huku akifunga juma ya mabao 13 katika jumla ya michezo 14 aliyocheza lakini akikabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa raia mwingine wa Ivory Coast Demba Ba.
Meneja wa Newcastle Alan Pardew.
No comments:
Post a Comment