Mshambuliaji wa Sevilla Alvaro ya Hispania ajiunga na Manchester City kuchukua nafasi ya Calos Teves.
Man City imekamilisha kumsajili mshambuliaji wa Sevilla Negredo kwa ada ya pauni milioni £24.5.
Alvaro Negredo alitarajiwa kukamilisha mpango huo hii leo jumatano mchana hii ikiwa ni kwa mujibu wa Rais wa Sevilla Jose Maria Del Nido.
Mapema wiki hii ilikuwa ikitazamiwa huenda mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania asingefanikiwa kuelekea nchini England kutokana na kwamba City isingefanikiwa kufikia kiwango hicho cha fedha lakini hatimaye vilabu hivyo viwili vimemaliza na kukata mzizi wa fitna.
City itaanza kulipa kwanza kiasi cha pauni milioni £21.5 kwa ajili ya uhamisho huo wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye aliifungia klabu yake jumla ya mabao 31 katika jumla ya michezo 42 aliyocheza msimu uliopita na baadaye City watamalizia pauni milioni £3.
Negredo ambaye alikuwepo katika kikosi cha Hispania kilicho shinda Euro 2012 anakuwa ni mchezaji wa pili kusajiliwa na City akitokea katika klabu ya Sevilla msimu huu baada ya kutanguliwa na Jesus Navas aliyehamia kwa pauni milioni £15.
Negredo
atakuwa akichukua nafasi ya Carlos Tevez aliyeelekea Juventus na huenda pia akaungana na Stevan Jovetic, wakati huu mazungumzo yakiendelea kwa ajili ya kujiunga na City kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £28 akitokea Fiorentina.
No comments:
Post a Comment