Taifa Stars
imeshindwa kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya leo (Julai 13 mwaka huu)
kufungwa bao 1-0 na Uganda (The Cranes) katika mechi ya kwanza ya mchujo
kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) zitakazofanyika
mwakani nchini Afrika Kusini.
Denis Iguma
ndiye aliyefunga bao hilo pekee kwa Uganda dakika moja baada ya mwamuzi Thierry
Nkurunziza kutoka Burundi kupuliza filimbi kuanzisha kipindi cha pili cha mechi
hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumzia matokeo hayo, Kocha wa Stars, Kim
Poulsen amesema mpira wa miguu ni mchezo wa kufunga mabao ambapo timu ilipata
nafasi nzuri katika dakika ya kwanza tu lakini ilishindwa kuibadili kuwa bao.
“Uganda walitengeneza nafasi moja tu katika
kipindi cha kwanza wakati sisi tulikuwa nazo kadhaa. Kipindi cha pili tuliwapa
nafasi wakafunga bao lao. Lakini kwa kifupi kama wao wameweza kufunga hapa (Dar
es Salaam), hata sisi tunaweza kufunga Kampala,” amesema Kim akizungumzia
nafasi ya timu yake kusonga mbele.
Timu
hizo zitarudiana jijini Kampala kati ya Julai 26 na 27 mwaka huu ambapo mshindi
ndiye atakayepata tiketi ya kwenda kwenye fainali za tatu za CHAN
zitakazofanyika Afrika Kusini. Stars ilicheza fainali za kwanza za CHAN zilizofanyika
mwaka 2009 nchini Ivory Coa
No comments:
Post a Comment