Timu ya Young Africans imewasili salama leo mchana mjini Tabora
ikitokea mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara yake ya
kutembeza Kikombe cha Ubingwa katika kanda ya Ziwa ambapo siku ya
alhamis inatarajiwa kucheza na timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro katika
uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mara baada ya kuwasili mjini Tabora timu ya Young Africans ilipata mapokezi makubwa kutoka kwa wapenzi, wanachama na washabiki wa timu hiyo kwa kuongozwa na msafara uliowaongoza mpaka katika hoteli ya Mwafrika waliyofikia.
Leo jioni kikosi cha Yanga kitafanya mazoezi katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo huo wa siku ya alhamis ambao utakua ni wa mwisho katika ziara hiyo ya kanda ya ziwa kabla ya timu kurejea jijini Dar es salaam siku ya ijumaa.
Mpaka sasa timu ya Young Africans imeshacheza michezo miwili dhidi ya timu ya Express kutoka nchini Uganda ambapo imetoka sare mmoja na kufungwa mchezo mmoja, ambapo mchezo wa keshokutwa itashuka dimbani kusaka ushindi kabla ya kuanza safari ya kurejea jijni Dar es salaam.

No comments:
Post a Comment