KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, August 14, 2013

MICHAEL CARRICK AUNGANA NA ASHLEY YOUNG KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA SCOTLAND.

Kiungo Michael Carrick ameondolewa katika kikosi cha timu ya taifa ya England kuelekea katika mchezo wa leo dhidi ya Scotland baada ya kupatwa na hitilafu ya jicho.

Kiungo huyo wa Manchester United mwenye umri w miaka 32 alitarajiwa kuitumia England kwa mchezo wa 30 mchezo ambao utapigwa katika dimba la Wembley.

Mchezo huo dhidi ya Scotland utakuwa ukichezwa zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya nchi hiyo Premier League.
Kiungo w Brighton, Liam Bridcutt amekumbwa na tatizo la msuli akiwa ni mchezaji pekee katika kikosi cha Scotland ambaye atakosekana hii.
Carrick atakuwa akiungana na Ashley Young kutoka Manchester United ambaye anasumbuliwa na matatizo ya kifundo cha mguu yaani 'ankle' ambao waliukosa mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Wigan ambao United ilishinda kwa bao 2-0.

No comments:

Post a Comment